Na. MUKSINI NAKUVAMBA –Mahakama, Mbeya
Watumishi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya wamekutana katika ukumbi wa
mikutano wa Mahakama Kuu kwa ajili ya hafla ya kuwakaribisha na kuwatambulisha
viongozi wapya waliohamia kuhudumu katika kanda hiyo.
Viongozi
waliokaribishwa katika hafla hiyo ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo
ya Mbeya Mhe. Benard Mpepo na Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya
Bw. Festo Chonya.
Hafla
hiyo, iliongozwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya
Mbeya, Mhe. Said Kalunde na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Mahakama Kuu,
Mahakimu wakiongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya,
Mhe. Teddy Mlimba, pamoja na watumishi wa Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu
Mkazi, Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo zilizopo Jijini Mbeya.
Akizungumza
katika kikao hicho, Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe.
Benard Mpepo alisisitiza umuhimu wa kujenga ushirikiano mzuri kati ya viongozi
na watumishi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi. .
Aidha,
aliwahimiza watumishi kuendelea kuendana na maboresho yanayoendelea kufanywa na
Mahakama ya Tanzania, hususan katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA, ambayo
imekuwa nyenzo muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za haki.
Kwa
upande wake, Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bw. Festo Chonya,
aliwahimiza watumishi kuendelea kudumisha upendo, kuheshimiana na kushirikiana
katika kutekeleza majukumu yao.
Pia
alisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, kuhakikisha
usafi na usalama wa miundombinu ya Mahakama, kutumia mifumo ya TEHAMA kwa
usahihi na kuwajibika kikamilifu katika maeneo yao ya kazi.
Hafla
hiyo pia, ilitoa fursa kwa wawakilishi wa watumishi kutoka katika kila Mahakama
kutoa salamu za ukaribisho kwa viongozi hao wapya na kuahidi ushirikiano katika
kutekeleza majukumu ya Mahakama.
Aidha,
hafla hiyo ya utambulisho na ukaribisho wa viongozi wapya ni hatua muhimu
katika kuimarisha mshikamano, kujenga uhusiano mzuri wa kikazi na kuweka msingi
wa ushirikiano kati ya viongozi na watumishi.
Vilevile,
hutoa fursa ya kuelekeza matarajio ya utendaji, kuimarisha uwajibikaji na
kuongeza ari ya pamoja katika kuboresha utoaji wa huduma za haki kwa wananchi
kwa kuzingatia maadili, ueledi na matumizi bora ya mifumo ya kisasa ya
Mahakama.
Kaimu
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Said
Kalunde (aliyesimama) akizungumza katika kikao hicho cha kuwakaribisha Viongozi,
kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya Bw. Festo Chonya, na
kushoto ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Mbeya Mhe. Benard Mpepo.
Naibu
Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Benard Mpepo akizungumza na
watumishi katika kikao hicho. (hawapo pichani) kulia ni
Mtendaji
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bw. Festo Chonya, akizungumza na
watumishi wa kanda ya Mbeya katika kikao hicho. (hawapo pichani)
Sehemu ya watumishi walioshiriki katika hafla fupi ya
kuwakaribisha Viongozi wapya wa Masjala Ndogo ya Mbeya wakifuatilia kwa makini shughuli
zilizokuwa zikiendelea katika kikao hicho.
Sehemu ya watumishi walioshiriki katika hafla fupi ya kuwakaribisha Viongozi wapya wa Masjala Ndogo ya Mbeya wakifuatilia kwa makini shughuli zilizokuwa zikiendelea katika kikao hicho.
Sehemu ya watumishi walioshiriki katika hafla fupi ya kuwakaribisha Viongozi wapya wa Masjala Ndogo ya Mbeya wakifuatilia kwa makini shughuli zilizokuwa zikiendelea katika kikao hicho
Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya Mbeya Mhe. Happines
Chuwa (aliyesimama) akitoa neno la shukurani katika kikao hicho kwa niaba ya
watumishi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni