Mahakama
ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kaliua- Tabora, Mhe. Anna Eliya Chilongola.
Kwa
mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, Bw.
Emmanuel Munda, marehemu Anna alifariki dunia tarehe 03 Julai, 2026 katika
Hospitali ya Mtakatifu Gemma mkoani Dodoma alipokuwa akipatiwa
matibabu.Amesema, msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe ‘Extension’-
Dodoma.
Bw.
Munda amesema kuwa, mazishi yanatarajia kufanyika tarehe 08 Julai, 2026 leo saa
7 Mchana katika Makaburi ya Chang’ombe jijini Dodoma.
Mahakama
ya Tanzania inaungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki katika kipindi hiki cha
majonzi ya kuondokewa na Mpendwa wetu Anna Eliya Chilongola.
BWANA
ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni