- Apata
pia fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo mafupi na Jaji Mkuu Masaju
Jaji Mstaafu wa Mahakama
ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe leo tarehe 08 Julai, 2026 ametoa
mada kwa Majaji wapya tisa wa Mahakama ya Rufani wanaoendelea kupatiwa Mafunzo
Elekezi ya kuwaandaa kuanza kutekeleza majukumu yao katika ngazi hiyo ya juu katika mfumo wa
utoaji haki nchini.
Mhe. Msoffe akiwa mmoja
kati ya Wawezeshaji wa Mafunzo hayo ametoa mada mbili ambazo ni Haki ya Msingi
dhidi ya Masharti ya Kiufundi na Maombi mbele ya Jaji mmoja wa Rufani na mbele
ya Jopo.
Mafunzo hayo ya siku tano
yanaendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania
jijini Dodoma.
Aidha, baada ya kutoa
mada hizo, Jaji Mstaafu Msoffe amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Jaji
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwake Makao
Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo,
Jaji Mkuu amemshukuru Mhe. Msoffe kwa kutenga muda wake na kufika kutoa mada
kwa Majaji hao wapya wa Mahakama ya Rufani.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyesimama mbele kushoto) akisalimiana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe mara baada ya Jaji Msoffe kutoa Mada kwa Majaji wapya tisa wa Mahakama ya Rufani leo tarehe 08 Julai, 2026 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni sehemu ya Majaji wapya tisa wa Mahakama ya Rufani wanaopatiwa Mafunzo Elekezi.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akizungumza jambo na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe alipomtembelea Jaji Mkuu leo tarehe 08 Julai, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza jambo na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe (hayupo katika picha) wakati Mhe. Msoffe alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 08 Julai, 2026.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe akimsikiliza Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (hayupo katika picha) alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 08 Julai, 2026.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiagana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe mara baada ya mazungumzo mafupi yaliyofanyika wakati Jaji Mstaafu Msoffe alipomtembelea Jaji Mkuu leo tarehe 08 Julai, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni