Jumatatu, 31 Agosti 2026

WATUMISHI MBEYA WAZURU HIFADHI YA NGORONGORO

Na MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya

Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya, wamefanya ziara ya kitalii katika Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha, ikiwa ni sehemu ya kuwapa fursa ya kupumzika, kujifunza, kutambua na kuthamini urithi wa asili na utamaduni wa Tanzania.

Ziara hiyo ya kitalii katika hifandhi ya Ngorongoro imeongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya, akiwa Pamoja na viongozi wengine wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Mbeya.

Akiongoza ziara hiyo, Mhe. Mtulya amesisitiza umuhimu wa watumishi kupata fursa za kujifunza na kutembelea maeneo mbalimbali, akieleza kuwa shughuli hizo zina nafasi katika kujenga mahusiano mazuri, kuimarisha mshikamano na kuongeza ari ya watumishi katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Viongozi walioshiriki katika ziara ya kitalii ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Benard Mpepo, Naibu Msajili Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Zawadi Laizer, Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bw. Festo Chonya, Mahakimu wakiongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbeya Mhe. Tedy Mlimba na watumishi wengine kutoka vituo mbalimbali vya Masjala Ndogo ya Mbeya.

Watumishi hao walipata fursa ya kutembelea na kujifunza kuhusu vivutio vya kiutalii vilivyopo katika eneo la Ngorongoro na kujionea wanyama na Ndege wa aina mbalimbali wanaopatikana katika hifandhi hiyo maarufu Duniani inayopatikana Tanzania.

Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni Bonde la Ngorongoro, eneo linalojulikana kwa utajiri wake wa wanyamapori na mandhari ya kipekee ya kijiolojia. Eneo la Ngorongoro pia ni miongoni mwa maeneo yenye hadhi ya urithi wa dunia kutokana na umuhimu wake wa asili, kiikolojia na kiutamaduni.

Watumishi hao pia walitembelea Ziwa Manyara pamoja na Makumbusho ya Ngorongoro–Lengai UNESCO Global Geopark, ambako walipata fursa ya kujifunza kuhusu historia, jiolojia, mazingira, utamaduni na namna ambavyo urithi wa asili unavyohifadhiwa na kutumika kwa ajili ya elimu na utalii.

Mbali na shughuli za utalii, ziara hiyo pia iliwawezesha watumishi hao kutembelea Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo Jumuishi cha utoaji haki Arusha, hatua iliyolenga kuwapa fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha mahusiano ya kikazi baina ya watumishi wa Mahakama kutoka Masjala hizo.

Ziara hiyo ya kiutalii imekuwa pia fursa ya kuwapa watumishi nafasi ya kujenga mshikamano, kuimarisha mahusiano baina yao na kupata muda wa kupumzika nje ya mazingira ya kawaida ya kazi, jambo linaloweza kuchangia kuongeza ari, morali na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ziara hiyo imehitimisha kwa kuwa fursa muhimu kwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya kujifunza zaidi kuhusu utajiri wa asili, historia, utamaduni na vivutio vya utalii vilivyopo nchini, huku wakijenga kumbukumbu na uzoefu ambao utachangia kuimarisha mshikamano na mahusiano yao ya kikazi.

Watumishi wa Mahakama ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya wakiwa mbele ya lango Kuu la kuingilia hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Picha na matukio mbalimbali ya Viongozi na Watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo y a Mbeya wakiwa katika ziara hiyo ya utalii katika hifadhi ya Ngorongoro.

Picha na matukio mbalimbali ya Viongozi na Watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo y a Mbeya wakiwa katika ziara hiyo ya utalii katika hifadhi ya Ngorongoro.

Viongozi na Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya wakiwa katika eneo la ziwa Manyara ambapo ilikuwa sehemu ya ziara hiyo ya kitalii.

Viongozi na Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya wakiwa mbele ya Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania, Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Arusha.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Benard Mpepo (kushoto) na Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, Bw. Festo Chonya (kulia) wakiwa mbele ya lango la kuingilia hifadhi ya ngorongoro walipotembelea katika hifadhi hiyo.

Watumishi wa Mahakama ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya wakipewa maelekezo na historia ya Hifadhi ya Ngorongoro kutoka kwa Mwongoza watalii (wa kwanza kushoto)

Picha na matukio mbalimbali ya Viongozi na Watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo y a Mbeya wakiwa katika ziara hiyo ya utalii katika hifadhi ya Ngorongoro.

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni