Na FRANCISCA SWAI – Mahakama, Musoma
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki, amezindua rasmi
utaratibu wa mazoezi kwa watumishi wa Mahakama Musoma kwa kuwasisitiza
kuzingatia utaratibu wa mazoezi ya mara kwa mara, kwani mazoezi ni afya, ajira,
furaha na ushirikiano.
Katika uzinduzi huo, Mhe.
Kakolak, amewashukuru viongozi wa Mahakama Sports Club Musoma kwa kuonesha
umahiri wao katika kusisitiza na kufuatilia suala hili.
Aidha, ametoa rai kwa
viongozi na watumishi kuhakikisha utaratibu huu wa mazoezi haupotei, bali uwe
endelevu kwa ajili ya kuimarisha afya za
watumishi ili waweze kufanya kazi zao kwa uadilifu, weledi na uwajibikaji.
Aidha, viongozi wa
Mahakama Sports Cub Musoma waliwasilisha taarifa yao iliyowashukuru viongozi chini
ya mlezi wao, ambaye ni Mtendaji wa Mahakama Musoma Bw. Leonard Maufi, kwa
kuwaunga mkono kutafuta Mwalimu wa Mazoezi na kusisitiza utaratibu huu wa
mazoezi kwa watumishi kuwa endelevu.
Pamoja na shukrani hizo,
walieleza mikakati mbalimbali ya michezo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na
kuandaa bonanza la michezo litakalohusisha Mahakama za jirani pamoja na wadau
mbalimbali wa Mahakama.
Uzinduzi wa program hii ya mazoezi umefanyika baada ya kuona faida za mazoezi kwa watumishi wa Mahakama Kuu Musoma ambao wamekuwa wakifanya mazoezi ya pamoja kila siku ya Jumanne na Alhamisi jioni.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (mwenye kofia), na
mbele yake ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma, Bw. Leonard Maufi, wakiwa katika
mazoezi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Musoma.
Watumishi wa Mahakama
wakiendelea na mazoezi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Musoma.
Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Tarime wakiwa katika mazoezi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Edwin Kakolaki (katikati), akiwa pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Marlin Komba (kulia) na Mhe. Kamazima Idd (kushoto) wakati akiongea na watumishi (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi rasmi wa mazoezi.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni