Na IMAN MZUMBWE - Mahakama, Songwe
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Songwe Mhe. Abubakar Amin Mrisha amefanya
ziara ya ukaguzi katika Gereza la Ngwala lililopo katika Wilaya ya Songwe mkoani
Songwe.
Ziara
hiyo iliambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya TEHAMA kama vile Televisheni
na Kamera kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma za Mahakama Mtandao ili kurahishisha
upatikanaji wa haki kwa wakati mapema ipasavyo kwa Wafungwa na Mahabusu wanaohifadhiwa mahala hapo.
Aidha,
Ukaguzi huo unatokana na utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Jaji Mfawidhi wa
Mahakama ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Malata alipofanya ziara
katika Gereza hilo miezi miwili iliyopita na kubaini changamoto ya usafiri kwa
wafungwa na mahabusu kutoka gerezani kwenda mahakamani kwa ajili ya
usikilizwaji wa mashauri yao.
“Tumekuja
kukabidhi vifaa vitavyosaidia kuweza kutatua changamoto ya usafiri kwa wafungwa
na mahabusu kutoka gerezani kwenda mahakamani kupitia matumizi ya vifaa vya TEHAMA
maarufu kama Mahakama mtandao,” alisema Mhe. Mrisha.
Mhe.
Mrisha alisema kuwa, matumizi ya Mahakama mtandao ni hatua muhimu katika
kuboresha utoaji huduma kwa wakati kwani teknolojia hiyo itawezesha baadhi ya
taratibu za kimahakama kufanyika kwa njia ya mtandao bila ulazima wa wafungwa na
mahabusu kusafirishwa kila mara kutoka gerezani kwenda mahakamani.
Kwa
upande, Afisa wa Magereza SP Kassim Akalama alisema kwamba, vifaa hivyo
vitasaidia kwa kiasi kikubwa usikilizwaji wa mashauri ya wafungwa na mahabusu
pamoja na gharama zingine zinazotumika katika kuwasafirisha kutoka gerezani
kwenda mahakamani.
SP
Akalama alisema kwamba, Jeshi la Magereza limepokea vifaa hivyo TEHAMA na
vitatumika kama ilivyokusudiwa, hatua hii ni muhimu kwani itasaidia kuboresha
huduma za utoaji haki kwa wafungwa na mahabusu na kuhakikisha haki inapatikana
kwa wakati mapema ipasavyo alisema afisa huyo wa magereza.
Ziara
hiyo ya kutembele na kukagua gereza hilo ni mwendelezo wa juhudi za Mahakama ya
Tanzania katika kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Magereza, huku matumizi ya
TEHAMA yakitarajiwa kuwa nyenzo muhimu katika kupunguza changamoto za utoaji haki
kwa wafungwa na mahabusu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni