Na MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Mbeya, Mhe. Fahamu Mtulya amekamilisha
ziara ya siku 14 ya kukagua na utambuzi wa Mahakama za Wilaya na Mwanzo kwa lengo
la kutathmini utendaji kazi, kubaini mafanikio, changamoto katika utoaji wa huduma
za haki pamoja na kuangalia hali ya miundombinu na mazingira ya kazi.
Ziara
hiyo iliyoanza tarehe 03 Septemba, 2026 na kuhitimishwa tarehe 16 Septemba,
2026 imehusisha kutembelea vituo vya Mahakama vilivyopo katika Wilaya za Kyela,
Rungwe, Mbarali, Chunya na Mbeya, ambapo jumla ya vituo 48 vilitembelewa,
vikiwemo vinavyotoa huduma na vile ambavyo kwa sababu mbalimbali havitoi huduma
kwa sasa.
Katika
ziara hiyo, Viongozi hao walifanya ukaguzi wa majengo, viwanja, mali za ofisi,
mazingira ya kazi na upatikanaji wa huduma za Mahakama, pia walitembelea maeneo
mbalimbali yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Mahakama.
Aidha,
ukaguzi huo umewezesha kubaini hali halisi ya vituo mbalimbali, ikiwemo baadhi
ya majengo chakavu, vituo ambavyo majengo yake hayatumiki au yameharibika,
pamoja na maeneo yenye viwanja pekee bila majengo ya Mahakama.
Ziara
imebaini hatua mbalimbali zinazochangia kuboresha utoaji wa huduma za haki ikiwemo
usikilizwaji wa mashauri kwa wakati, matumizi ya mfumo wa ‘Primary Court App’
katika Mahakama za Mwanzo, upatikanaji wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu, ukarabati mdogo wa majengo na vifaa vya Ofisi, pamoja na kuimarika
kwa ushirikiano kati ya Mahakama na wadau mbalimbali.
Katika
baadhi ya vituo, ziara imebaini mafanikio katika kufunga mirathi kwa wakati,
utoaji wa nakala za hukumu na mienendo kwa wakati, utoaji wa elimu kwa umma,
pamoja na kuendelea kwa jitihada za kuimarisha mazingira ya utoaji wa huduma za
haki.
Hata
hivyo, ukaguzi umebaini changamoto zinazohitaji hatua za kimkakati, zikiwemo
uchakavu wa baadhi ya majengo yanayotumika kutoa huduma za kimahakama, upungufu
wa watumishi, ukosefu wa huduma muhimu kama maji katika baadhi ya vituo,
upungufu wa Samani za ofisi, pamoja na baadhi ya viwanja vya Mahakama kutokuwa
na hati miliki na alama za kudumu za mipaka.
Viongozi
hao kupitia ziara hiyo, walitoa maelekezo mbalimbali kwa uongozi wa vituo
husika, yakilenga kuharakisha hatua za upatikanaji wa hati na alama za mipaka
ya viwanja, kuboresha miundombinu, kuongeza kasi ya usikilizwaji na
ukamilishaji wa mashauri, kutoa nakala za hukumu kwa wakati, pamoja na
kuimarisha usimamizi wa karibu wa utendaji kazi wa Mahakama.
Aidha,
katika vituo ambavyo huduma za Mahakama hazipatikani, viongozi walifanya tathmini
ya sababu za kutokuwepo kwa huduma hizo na kutoa maelekezo yanayolenga kuweka
mazingira wezeshi ya kurejesha au kuimarisha huduma, ikiwemo kuhamasisha
ushirikiano na Serikali za Vijiji na wadau wengine katika ujenzi wa majengo ya
Mahakama.
Uongozi
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya utaendelea kufuatilia utekelezaji wa
maelekezo yaliyotolewa katika vituo mbalimbali, kwa lengo la kuhakikisha
maboresho yaliyobainika yanatekelezwa na huduma za haki zinaendelea kutolewa
kwa ufanisi, kwa wakati na katika mazingira yanayokidhi mahitaji ya wananchi na
watumishi wa Mahakama.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), na
viongozi wengine alioambatana nao katika ziara hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja
na Wadau na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Madibira alipotembelea Mahakama
hiyo alipokuwa ziarani wilayani Mbarali.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) na
viongozi wengine alioambatana nao katika ziara hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja
na Watumishi wa Mahakama ya Watoto Mbeya.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akiwa ndani ya
Ofisi ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Rungwe, alipotembelea
alipokuwa katika ziara hiyo.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (kulia),
akikagua miundombinu ya TEHAMA katika Chumba cha TEHAMA Mahakama ya Mwanzo
Madibira.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), na
viongozi wengine alioambatana nao katika ziara hiyo wakipokelewa na watumishi
wa Mahakama ya Wilaya ya Chunya na Mahakama ya Mwanzo Chunya Mjini.
Watumishi
wa Mahakama ya Wilaya Chunya na Mahakama ya Mwanzo Chunya Mjini wakimsikiliza Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (hayupo
pichani), ndani ya ukumbi wa Mahakama ya Wilaya Chunya.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya na viongozi
wengine alioambatana nao katika ziara hiyo wakikagua viwanja na maeneo
mbalimbali ya yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo katika
wilaya mbalimbali walizotembelea katika ziara hiyo.

viongozi wengine alioambatana nao katika ziara hiyo pamoja na viongozi wa
Mahakama ya Wilaya Chunya na Diwani wa Kata ya Makongorosi (watatu kushoto)
wakiwa mbele ya jengo la Mahakama ya Mwanzo Mkongorosi linalojengwa na nguvu ya
Wananchi na wadau mbalimbali wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni