Alhamisi, 22 Oktoba 2026

JAJI MKUU MASAJU AFANYA ZIARA MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA ARDHI

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 22 Oktoba, 2026 ametembelea Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo fupi, Mhe. Masaju amefanya mazungumzo na Watumishi wa Mahakama hiyo kuhusu masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha zaidi huduma ya utoaji haki nchini.

Kadhalika, katika mazungumzo hayo, Jaji Mkuu amewapongeza Watumishi wote wa Mahakama hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya.

Yafuatayo ni matukio katika picha ya ziara ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju alipotembelea Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi-Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akisalimiana na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi alipowasili katika Mahakama hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Oktoba, 2026  kwa ziara ya kikazi. Wa kwanza kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Elinaza Luvanda.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Elinaza Luvanda (aliyesimama) akimkaribisha na kutoa taarifa ya Mahakama hiyo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele). Walioketi ni baadhi ya Majaji wa Divisheni hiyo.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza na Watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi leo tarehe 22 Oktoba, 2026 alipotembelea Mahakama hiyo.

Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi wakifurahia jambo wakati Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (hayupo katika picha) alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Mahakama hiyo alipofanya ziara ya kikazi leo tarehe 22 Oktoba, 2026 jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya Majaji na Watumishi wengine wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi wakimsikiliza Jaji Mkuu, Mhe. Masaju (hayupo katika picha) alipokuwa akizungumza nao leo tarehe 22 Oktoba, 2026 alipotembelea Mahakama hiyo.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi (hawapo katika picha). Aliyeketi kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divsiheni ya Ardhi, Mhe. Elinaza Luvanda na kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Mohamed Gwae.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divsiheni ya Ardhi, Mhe. Elinaza Luvanda akizungumza jambo wakati Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (hayupo katika picha) alipotembelea Mahakama hiyo leo tarehe 22 Oktoba, 2026 jijini Dar es Salaam.

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Bw. Donald Makwaia akizungumza jambo wakati Jaji Mkuu alipotembelea Mahakama hiyo leo tarehe 22 Oktoba, 2026 jijini Dar es Salaam. Aliyeketi kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Niku Mwakatobe.


Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi katikati) akiwa katika picha za pamoja na Majaji, Naibu Wasajili, Watendaji na sehemu ya Watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi. Aliyeketi kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divsiheni ya Ardhi, Mhe. Elinaza Luvanda na kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Mohamed Gwae.

(Picha na BAKARI MTAULLAH)
































 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni