Jumamosi, 24 Oktoba 2026

JAJI TIGANGA APOKEA UGENI WA NAIBU WAKILI MKUU WA SERIKALI

Na ARAPHA RUSHEKE

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, tarehe 22 Oktoba, 2026 alipokea ugeni kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Dodoma.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo, alimtembelea Mhe. Tiganga wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mkoani Dodoma.

Viongozi hao walijadili masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya kazi, kuimarisha ushirikiano baina ya Taasisi hizo pamoja na kuboresha mahusiano ya kikazi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za haki kwa wananchi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga, akisikiliza jambo mara baada ya kupokea ugeni wa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi Alice Mtulo (hayupo pichani).

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi Alice Mtulo, akisikiliza jambo mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Jaji Mfawidhi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe Joachim Tiganga (wa kwanza   kushoto) akifurahia jambo na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi Alice Mtulo wakati wa mazungumzo yao.

Sehemu ya Viongozi wa Mahakama Kuu Dodoma pamoja na sehemu ya wajumbe kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakifuatilia kwa umakini mazungumzo hayo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga (aliyepo katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake. Kushoto kwake ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi Alice Mtulo na kulia kwake ni Naibu Msajili wa Mahakama, Mhe Upendo Ngitiri.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Joachim Tiganga (wa kwanza kulia akiagana na Naibu wakili Mkuu wa Serikali, Bi Alice Mtulo aliemtembelea.

 

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni