Na AIDAN ROBERT, Mahakama-Kigoma
Mwenendo wa matumizi ya fedha za kuendeshea shughuli za
Mahakama imeelezwa kuwa zinatumika vema katika shughuli za Mahakama Kanda ya
Kigoma kupitia vipaumbele muhimu vilivyowekwa kuwezesha upatikanaji haki mapema
ipasavyo.
Hayo yalibainishwa wakati wa Kikao cha Bajeti ya Kanda ya
Kigoma kilichofanyika tarehe 23 Oktoba 2025, kilichoongozwa na Mtendaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Bw. Yusufu Kasuka kwenye ukumbi wa Mahakama ya
Wilaya Kakonko mkoani Kigoma.
Akitoa neno la ufunguzi wa kikao hicho, Bw. Kasuka alisema
kuwa,
mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa bajeti iliyopita,
huku akisisitiza umuhimu wa uwazi na matumizi sahihi ya rasilimali za umma na
katika kuweka mikakati ya mwaka mpya wa fedha, msisitizo mkubwa umewekwa kwenye
kuboresha mazingira ya utoaji haki, kusogeza huduma karibu na wananchi na
kuhakikisha mashauri yanasikilizwa mapema ipasavyo.
Vilevile, aliwakumbusha wajumbe
kuwa, wananchi wanategemea huduma bora kutoka mahakamani, hivyo uwajibikaji na
uadilifu vinapaswa kuwa mstari wa mbele.
"Tunapokea mwaka mpya
wa fedha kwa mtazamo chanya. Lengo letu kuu ni kuondoa mkwamo wowote wa
kimaendeleo na kiutendaji, kuhakikisha haki inatolewa mapema ipasavyo, na
kusimamia vema rasilimali zetu kwa ustawi wa Mahakama yetu ya Kigoma." alisema
Bw. Kasuka.
Aidha, alisisitiza kwamba, matumizi ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaendelee kushika kasi maana ndio muelekeo wa
Mahakama ya Tanzania, hivyo watumishi wote Kanda ya Kigoma wawe na bidii katika
matumizi ya vifaa vya TEHAMA na kuvitunza kwakuwa mwajiri anajitahidi
kuhakikisha kila mtumishi anakuwa na kifaa chake cha kutumia katika majukumu
yake ya kila siku.
Katika kikao hicho, Kamati ya Bajeti iliazimia kuhakikisha
fedha za mirathi zilizopo katika akaunti ya Mahakama zinalipwa kwa wadaawa na
jumla ya mirathi 27 zimetambuliwa na kulipa fedha hizo kwa wahusika wa mirathi
hizo, na kwamba imebainishwa kuwa, zoezi la utambuzi wa fedha za mirathi
unaendelea ili kumaliza kabisa wingi wa fedha za mirathi zilizopo katika
akaunti ya Mahakama Kigoma.
Kwa upande wake, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Masjala Ndogo Kigoma, Mhe. Fadhili Mbelwa amewapongeza Maofisa Bajeti wa
Mahakama za Wilaya kwa taarifa nzuri za utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha
2025/2026-2026/2027, kwani imegusa vipaumbele vya Mahakama, imetekelezwa kwa
ufanisi mkubwa kwa usikilizwaji wa mashauri na utatuzi wa changamoto kutumia
rasilimali fedha ndogo inayopatikana.
Mhe. Mbelwa alitumia fursa hiyo kuwasisitiza Mahakimu
Wakazi Wafawidhi wa Wilaya zote ndani ya Mkoa huo kuendelea kusimamia vema
bajeti zao ili zifanye shughuli muhimu za Mahakama kama Mpango Mkakati wa Mahakama
unavyoelekeza.
Wajumbe wa kikao hicho walikuwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Wilaya, Wakuu wa Idara za Mahakama Kuu Kigoma na Maofisa Tawala kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Mahakama za Wilaya Kigoma, Kibondo, Uvinza, Kasulu, Buhigwe na Kakonko.
Mtendaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Kigoma, Bw. Yusufu Kasuka akisisitiza jambo wakati wa
kikao cha bajeti kilichofanyika tarehe 23 Oktoba, 2026 kwenye ukumbi wa Mahakama ya Wilaya Kakonko.
Naibu
Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Kigoma, Mhe. Fadhili Mbelwa akisisitiza jambo
wakati wa kikao cha bajeti kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mahakama ya wazi Wilaya Kakonko.
Sehemu ya Wajumbe wa Kikao cha Bajeti wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya Wajumbe wa Kikao cha Bajeti wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea katika kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe wa Kikao cha Bajeti katika wakifuatilia kwa umakini mjadala uliokuwa ukiendelea wakati wa Kikao cha Bajeti ya Mahakama Kigoma.
Wajumbe wa Kikao cha Bajeti Mahakama Kigoma.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Masjala Ndogo Kigoma, Bw. Yusufu Kasuka (katikati) pamoja na Naibu Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Kigoma, Mhe. Fadhili Mbelwa (kushoto) na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma Mhe. Aristida Tarimo (aliyeketi kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wengine wa Kikao cha Bajeti ya Mahakama Kigoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mahakama ya Wilaya Kakonko.
(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Serengeti)







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni