Jumanne, 6 Oktoba 2026

MKUTANO WA SEACJF WAENDELEA KUFANYIKA ZANZIBAR

Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu kutoka Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) uliofunguliwa jana tarehe 05 Oktoba, 2026 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi unaendelea kufanyika Visiwani humo.

Leo tarehe 06 Oktoba, 2026 ikiwa ni siku ya pili ya Mkutano huo muhimu unaofanyika katika Hoteli ya Verde Visiwani humo, Mada mbalimbali zimeendelea kutolewa sambamba na kubadilishana uzoefu miongoni mwa Wakuu hao wa Mahakama kutoka Ukanda huo.

Mada zilizotolewa ni pamoja na ya Mabadiliko ya Kidijitali katika Mahakama: Uwasilishaji wa Kielektroniki wa Nyaraka, Usikilizaji wa Kesi kwa Njia ya Mtandao, na Mifumo ya Usimamizi wa Mashauri (Digital Transformation of Courts: E-filing, Virtual Hearings, and Case Management Systems Digital Transformation of Courts: E-filing, Virtual Hearings, and Case Management Systems) na nyingine.

 Matukio katika picha, Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) unaofanyika Hotel Verde Visiwani Zanzibar.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia), Jaji Mkuu wa Namibia, Mhe. Peter Shivute (katikati), Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Martha Koome (kusoma) pamoja na Washiriki wengine wanaoshiriki katika Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Kusini na Mashariki mwa Afrika unaofanyika katika Hoteli ya Verde Visiwani Zanzibar.

Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania (walioketi mbele) wakiwa katika Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) unaoendelea kufanyika Hoteli Verde Visiwani Zanzibar. Kulia ni Mhe. Ruth Massam na kushoto ni Mhe. Gladys Barthe.


Washiriki wa Mkutano wakifuatilia kinachojiri katika Mkutano wa SEACJF unaoendelea kufanyika katika Hoteli ya Verde Visiwani Zanzibar.

(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Zanzibar)




 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni