Jumapili, 4 Oktoba 2026

WATENDAJI WAKUU WA MAHAKAMA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA WAKUTANA ZANZIBAR

Na MARY GWERA, Mahakama-Zanzibar

Watendaji Wakuu  wa Mahakama kutoka Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) akiwemo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu leo tarehe 04 Oktoba, 2026 wamekutana na kufanya Mkutano wa majadiliano wenye lengo la kujadili utendaji wao kwa nia ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za Mahakama kwa wananchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Verde Visiwani Zanzibar.

Aidha; Watendaji Wakuu hao wa Mahakama watashiriki katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) utakaofanyika visiwani humo kwa siku tano kuanzia tarehe 05 hadi 09 Oktoba, 2026.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano huo uliokusanya zaidi ya Majaji Wakuu 15 pamoja na Viongozi na Wadau wa Sheria kutoka nchi hizo.

Matukio katika picha Mkutano wa Watendaji Wakuu wa Mahakama kutoka Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) uliofanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2026 Visiwani Zanzibar.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu (kulia) akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Chama cha Watendaji Wakuu wa Mahakama kutoka Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) uliofanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2026 katika Hoteli ya Verde Visiwani Zanzibar.


Picha mbalimbali za Watendaji Wakuu wa Mahakama wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika wakiendelea na Mkutano wao uliofanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2026 katika Hoteli ya Verde Visiwani Zanzibar.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Kenya, Mhe. Winifrida Mokaya akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Chama cha Watendaji Wakuu wa Mahakama kutoka Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika uliofanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2026 Visiwani Zanzibar.

Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia kwa umakini kilichokuwa kikijiri katika Mkutano wa Chama cha Watendaji Wakuu wa Mahakama wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) uliofanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2026-Zanzibar.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni