Jumatano, 18 Novemba 2026

JAJI MSTAAFU EUSEBIA MUNUO AMTEMBELEA JAJI MKUU MASAJU

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo jana tarehe 17 Novemba, 2026 alimtembelea Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju na kupata fursa ya kufanya naye mazungumzo mafupi ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.  

Kadhalika, Mhe. Munuo aliwasili Makao Makuu ya Mahakama ili kushiriki katika Hafla ya Uzinduzi wa Kitabu chake kiitwacho JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania” kilichozinduliwa na Jaji Mkuu.

Matukio katika picha, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Munuo alipotembelea Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju tarehe 17 Novemba, 2026 Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.


Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akisalimiana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo (kulia) alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2026. Kushoto  ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2026.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo (kushoto) akifanya mazungumzo na 
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2026.

Mazungumzo yakiendelea. Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Amidi wa Mahakama hiyo, Mhe. Augustine Mwarija.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo (wa pili kushoto). Wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Amidi wa Mahakama hiyo, Mhe. Augustine Mwarija na wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiagana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo.

(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)




 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni