Jumatano, 1 Mei 2024

WATUMISHI MAHAKAMA DAR ES SALAAM WASHIRIKI MAADHIMISHO MEI MOSI 2024

Na FAUSTINE KAPAMA -Mahakama, Dar es Salaam


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Dar-es-Salaam, leo tarehe1Mei, 2024 wameungana na Watanzania wengine kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi, inayojulikana kama Mei Mosi, inayosherekewa kote duniani.

 

Maadhimisho hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila yamefanyika katika Uwanja vya Uhuru jijini hapo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

 

Pilikapilika za maadhimisho hayo zilianza mapema asubuhi ambapo watumishi wa Mahakama waliojitokeza kwa wingi waliungana na wananchi wengine katika eneo la Mnazi Mmoja na baadaye kushiriki kwenye maandamano hadi kwenye Uwanja wa Uhuru.

 

Maandamano hayo yaliyoongozwa na Bendi ya Jeshi la Magereza yalipita katika barabara ya Nyerere, Keko na baadaye Uwanja wa Uhuru na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa.

 

Watumishi wa Mahakama ya Tanzania ndiyo waliokuwa wa kwanza kuingia katika Uwanja wa Uhuru na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi waliofurika uwanjani hapo kufuatia kazi nzuri wanayoifanya katika muktadha mzima wa utoaji haki nchini.

 

Mhe. Chalamila aliongoza jukwaa kuu kuwashangilia watumishi wa Mahakama walipokuwa wanapita mbele yake na kupokewa na wananchi wengine waliokuwa wamesimama muda wote.

 

Mbali na watumishi kupita mbele ya mgeni rasmi kwenye maandamano hayo, magari ya Mahakama nayo yalikuwa miongoni kutoka Taasisi na mashirika mbalimbali ambayo yalipita mbele yake, likiwemo gari la Mahakama Inayotembea, ‘Mobile Court’, ambalo lilikuwa kivutio kikubwa kwa wananchi.

 

Baada ya maandamano hayo, ratiba ya maadhimisho hayo iliendelea, ikiwemo viongozi mbalimbali wa Chama cha Wafanyakazi (TUCTA) na Serikali ya Mkoa walipata nafasi ya kutoa salamu.

 

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Chalamila amewapongeza wafanyakaizi wote kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu wa 2024 yamebeba kauli mbiu inayosema, “Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinda dhidi yahali ngumu ya maisha.”

 


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Dar-es-Salaam wakijiandaa kushiriki katika maandamano kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Dar-es-Salaam wakiingia kwenye Uwanja wa Uhuru kushiriki katika maandamano kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Dar-es-Salaam (juu na chini) wakipita mbele ya jukwa kuu, likiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, leo tarehe 1 Mei, 2024 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.


Jukwa Kuu, likiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila likiwapungia mkono watumishi wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam walipokuwa wanapita mbele yake katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania nao hawakubaki nyuma kushiriki kwenye maadhimisho hayo.

Bendi ya Jeshi la Magereza iliyoongoza maandamano hayo ikipita mbele ya mgeni rasmi kwenye Uwanja wa Uhuru.

Sehemu ya magari ya Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Dar-es-Salaam (juu na picha mbili chini) ikipita ndani ya Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwenye maadhimisho ya Mei Mosi.

 


Sehemu ya Wananchi wa Mkoa wa Dar-es-Salaam (juu na chini) waliojitokeza  kwenye maadhimisho ya Mei Mosi.  

Watumishi wa Mahakama ya Tanzania, Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja (juu na chini) kabla ya kupanda magari kuelekea kwwenye maadhimisho ya Mei Mosi.



Safari ndiyo inaanza. 

 




 


 


 


 


 


 

Safari kuelekea katika maeneo ya Mnazi Mmoja ndiyo inaanza kushiriki katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.

 

Sehemu ya magari ya Mahakama ya Tanzania yakiwa yamefurika watumishi yakiwasili katika maeneo ya Mnazi Mmoja kabla ya kuanza maandamano hayo.

 

Maandamano yameanzia sasa.

 

Maandamano yamekolea....

 


 

 

Wananchi wakiimba wimbo wa mshikamano katika Uwanja wa Uhuru baada ya maandamano.

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni