Jumatano, 24 Septemba 2025

WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

NA DOTTO NKAJA- Mahakama, Geita

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 22 Septemba, 2025 alizindua Maonyesho ya nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini Mkoa wa Geita kwa mwaka 2025 na baadaye kukagua mabanda mbalimbali yaliyowekwa na Wadau, ikiwemo Mahakama.

Mhe. Majaliwa aliweza pia kutembelea Banda la Mahakama Kuu, Masjala ya Geita na kupokelewa na MJaji Mfawidhi, Mhe. Kevin Mhina. Mhe. Waziri Mkuu aliweza kujionea jinsi Mahakama inavyotoa huduma ya elimu ya kisheria kwa wananchi wanaofika kutembelea maonesho hayo.

Waziri Mkuu alimpogeza Jaji Mfawidhi kwa kuwa sehemu ya Wadau waliojitoa kutoa elimu kwa Umma mkoni Geita. “Hii inaonesha dhamira ya dhati kabisa kwa Mahakama kuwafikia wananchi na kuhakikisha wanapata elimu ya kisheria,” alisema.

Naye Jaji Mfawidhi alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutembelea Banda la Mahakama Kuu na kujionea jinsi Mahakama inavyojipambanua katika kuwafikia wananchi kwa kutoa elimu bure kipindi chote cha maonesho.

Maonesho ya madinikatika  Mkoa Geita hufanyika kila mwaka mwezi tisa yakiwa na lengo la kukuza biashara ya madini na kuwahamasisha wananchi kwenye matumizi sahihi ya teknologia katika uchimbaji wa madini, hivyo kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja.

Manensho haya yanategemewa kuhitmishwa tarehe 28 Septemba, 2025.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na kufanya mazungumuzo mafupi na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Geita, Mhe. Kevin Mhina katika banda la Mahakama.

Picha ya pamoja katika banda la kutolea elimu la Mahakama Kuu Kanda ya Geita, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mhakama ya Tanzania, Kanda ya Geita, Mhe. Kevi Mhina, wa tatu kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Geita, Mhe. Fredrick Lukuna, wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Geita, Bi. Masalu Kisasila na Mahakimu wengine.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akielekeakwenye Banda la Mahakama katika uzinduzi wa Maonyesho ya 8 Kitaifa ya Madini Mkoa wa Geita 2025.

Wananchi wakipata ufafanuzi wa kisheria kwa Mhe. Ally Mgomba katika banda la Mahakama Kuu Kanda ya Geita.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Geita, Mhe. Fredrick Lukuna akiwatoa hofu wananchi kuwa mahakamani ni sehemu ya haki na salama.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni