Jumatano, 16 Desemba 2015

JAJI MKUU WA TANZANIA, MHE. MOHAMED CHANDE OTHMAN AWAAPISHA JUMLA YA MAWAKILI 104 KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM. TAREHE 15/12/2015.





Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika meza kuu pamoja na Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani, na Mahakama Kuu ya Tanzania katika sherehe za kuwakubali na kuwasajili Mawakili Wapya, mkatika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisoma risala yake katika sherehe hizo ambapo amewataka Mawakili hao wapya kuwawakilisha vyema wananchi katika kupata haki zao.


 
Ni kundi la baadhi ya Mawakili waliosajiliwa leo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 

Wakitoa heshima ya Kimahakama mbele ya Mhe. Jaji Mkuu na Majaji wengine wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria katika sherehe hiyo.

 
 
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahe Majaji wa Mahakama ya Rufani (walioketi), Mhe. Shaaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa tatu kulia) na baadhi ya Mawakili wapya (waliosimama) waliopishwa.
 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni