Simon Berege, Mwenyekiti wa MISA-TAN Afrika, (wa saba
kulia), katika picha ya pamoja na watoa mada, Wasaidizi wa Kumbukumbu
Mahakama ya Tanzania walioshiriki mafunzo ya Huduma kwa Wateja, Mkoani Morogoro.
Mafunzo
maalumu ya siku mbili yahusuyo huduma kwa wateja na haki ya kupata taarifa kwa watumishi
wa Mahakama, yameanza leo katika hoteli ya Flomi mkoani Morogoro ikiwa ni
muendelezo wa mafunzo yaliyozinduliwa mwaka jana na Jaji Mfawidhi Kanda ya
Dodoma Mhe. Crecensia Makuru.
Lengo
Kuu la mafunzo haya likiwa ni kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama kwa kuwapa
mbinu na mikakati mbalimbali itakayowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji
kazi.
Mahakama
ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya utendaji kazi wake kama sehemu
ya kuhakikisha kuwa inatoa huduma iliyo bora na kwa wakati. Moja ya maeneo
yaliyoonekana kuwa na udhaifu ni namna masijala za Mahakama zinavyopokea na
kutunza nyaraka na hata zinavyohudumia wateja kwa ujumla.
Walengwa wa mafunzo haya ni watumishi wa kada mbalimbali za mahakama
wakitokea kanda ya Mashariki inayounganisha mikoa ya Pwani, Dodoma, Dar es
Salaam na Morogoro.
Miongoni
mwa mada zinazowasilishwa ni “Nini maana ya uhuru wa Habari na habari ni Nini?,
Huduma kwa wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa watumishi wa Umma, Njia mbalimbali
za upatikanaji wa taarifa katika Taasisi za Umma na Sheria ya utoaji wa habari katika Mahakama”.
Mafunzo
haya yameandaliwa na kufadhiliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) pamoja na Taasisi ya
Friedrick Ebert Stiftung (FES) ofisi ya Tanzania.
Watumishi
wa Kada mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria mafunzo ya Huduma kwa
wateja ili kuweza kuwajengea ujuzi na ufanisi katika kazi mahakamani.
Simon Berege,
Mwenyekiti wa MISA-TAN Afrika, akielezea umuhimu wa mafunzo ya huduma kwa
wateja hasa kwa watumishi wa Mahakama ili kuweza kutoa taarifa sahihi ambazo
zitarahisisha kutoa haki na kwa wakati
Deus
Kibamba, Mkurugenzi wa TCIB, (aliyesimama ) akifundisha mada
ya “Nini maana ya uhuru wa Habari na habari ni Nini.
James Marenga, Wakili wa Mahakama
Kuu na Mwanahabari, (aliyesimama) akifundisha juu ya “Uboreshaji wa huduma bora kwa wateja”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni