Jumapili, 31 Januari 2016

UFUNGUZI WA WIKI YA SHERIA KWA MWAKA 2016.


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa maandamano  jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwa mwaka 2016.


 

Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.


  

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.
 
 
Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya Wadau wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini jijini
 Dar es salaam.
 

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza na wadau mbalimbali wa Mahakama waliohudhuria Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwa mwaka 2016  katika viwanja vya Mnazi mmoja  jijini Dar es salaam.
 
 
Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria. Wengine katika picha hiyo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kutoka kushoto).
 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watendaji wa Mahakama, Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria jijini Dar es salaam.
 
 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo katika viwanja vya Mnazi Mmmoja wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Watendaji na Watumishi wa Mahakama ya Zanzibar.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akiwa katika picha ya pamoja na Wasajili, Wakuu wa Idara na Watumishi  mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.
 
 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akiwa na viongozi wa Mahakama ya Tanzania katika picha ya pamoja na Askari wa Jeshi la Magereza wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria.
 
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa na Wasajili na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania Mkoani  Dar es salaam katika picha ya pamoja wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria kwa mwaka 2016.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa na meza kuu katika picha ya pamoja na Mawakili na Watumishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).


 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni