Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe
(kushoto) akimkabidhi Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es salaam
Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa
na Mahakama ya Tanzania.
Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe
(kushoto) akishirikiana na Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es
salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) kupakua msaada wa vyakula na vitu mbalimbali
vilivyotolewa na Mahakama ya Tanzania.
Jamii
imeaswa kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu na makundi yenye mahitaji maalumu
hususan wafungwa walio magerezani na wasiojiweza ili kudumisha upendo na kuyafanya makundi
hayo kujiona yanathaminiwa katika jamii.
Wito
huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano Mahakama ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe wakati akikabidhi msaada
wa vyakula na vitu mbalimbali kwa Mahabusu ya Watoto ya jijini Dar es salaam
vilivyotolewa na Mahakama ya Tanzania kama zawadi yao ya mpya 2016..
Bw.
Ndimbe amesema Mahakama ya Tanzania imetoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo
Mchele, Sabuni, Vinywaji, Chumvi, Unga wa Ngano, Unga wa Sembe, Mchele ,Sukari
na Mafuta ya kupikia kwa Mahabusu hao kuonyesha
Upendo na namna Mahakama hiyo inavyowathamini watoto hao.
Ameongeza
kuwa Mahakama ya Tanzania imetoa msaada huo kwa lengo la kujenga mahusiano
mema baina yake na watoto hao ili waendelee kuipenda na kuwa na mtazamo chanya
juu ya utendaji wake.
‘
Nimekuja kukabidhi msaada huu kwa niaba ya Mahakama ya Tanzania kwa
Mahabusu hii ya Watoto ikiwa ni zawadi yao ya mwaka mpya, lengo letu ni kujenga
mahusiano mema kati yetu Mahakama na watoto hawa wajue kuwa tunasaidia jamii
katika masuala mbalimbali’’ Amesema Bw. Ndimbe.
Kwa
upande wake Afisa Mfawidhi wa Mahabusu hiyo Bw. Ramadhan Yahaya akizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo ameishukuru Mahakama ya Tanzania kwa uamuzi
wake wa kuwakumbuka Mahabusu hao.
Amesema
kitendo cha Mahakama ya Tanzania kuwapatia msaada huo kimewapa faraja
watoto hao na kuwafanya wajione wanathaminiwa na kupendwa na Mahakama hiyo.
Ametoa
wito kwa Taasisi na Mashirika mengine kuiga mfano huo ulioonyeshwa na Mahakama ya Tanzania ili kudumisha upendo miongoni mwa makundi ya watu wenye
mahitaji maalum.
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni