Kwa mujibu wa Kifungu
107 (A) Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa
Mahakama. Na kazi kubwa ya Mahakama kama mhimili ni kutafsiri sheria
zilizotungwa na Bunge.Kwa wananchi walio wengi kazi ya vyombo vya habari ni
kama Mahakama kwa maana ya ukweli kuwa habari hutumika kwa ukweli na uhakika
kwa wananchi.
Tarehe 2 na 3 Mei 2016 itakumbukwa na
Wanahabari wengi nchini kwa kuadhimisha siku ya muhimu ya Uhuru wa vyombo vya
Habari Duniani. Madhimisho hayo yaliyofanyika katika Hoteli maarufu ya Malaika
Beach Resort jijini Mwanza, yaliambatana na maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio
la Windhoek lilioridhia kuanzishwa kwa Tasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika
yaani (MISA). Wanahabari waliadhimisha pia miaka 250 ya sheria ya kwanza ya
kupata taarifa ikijumuisha nchi ya Sweden na Finland. Kadhalika kongomano hilo
la siku mbili lilitathimini mafaniko ya mwaka wa kwanza wa miaka 15 ya
utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Millenia (Sustainable
Development Goals (SDGs) ya Umoja wa
Mataifa.
Katika kongomano hilo la Uhuru wa
vyombo vya Habari Duniani mgeni rasmi alikuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed
Chande Othman, ambaye katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Jaji
mfawidhi Mahakama Kuu kanda ya Mwanza Mhe.Robert Makaramba alielezea umuhimu wa
Mahakama kuheshimu Uhuru wa vyombo vya habari katika mustabali wa kuleta
demokrasia ya kweli nchini. Aidha Mhe.
Jaji Mkuu aliendelea kwa kuwauliza wanahabari ni kwa kiasi gani vyombo vya
habari huripoti habari za maendeleo,haki za binadamu, masuala ya utawala bora?.
Na vipi Wahariri wetu hupima ubora wa habari zinazoandikwa katika magazeti yetu
na je kiandikwacho kinaweza kuleta mabadiliko kwa mtu atakayesoma,kusikiliza,ama
kuona habari hiyo?
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza Mhe. Robert Makaramba (aliyesimama) akisoma hotuba kwa niaba ya Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman wakati ufunguzi wa Komngomano la
Sikiu ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani katika Hotel ya Malaika Beach Resort
Jijini Mwanza.
Maswali haya yaliibua mjadala kuhusu haki
ya kupata habari na uhuru wa vyombo vya habari kwa ujumla. Mhe.Jaji mkuu alileeza
kuwa, Mahakama kama mdau wa habari inashauri
wanahabari kupambana na changamoto zilizopo katika kuwasilisha habari za
aina tofuti. ‘’ Kuna changamoto kubwa katika kauandika habari zinazohusu haki
za binadamu. Kwa siku za karibuni suala la haki za binadamu limekuwa likipigwa
chapuo na wadau wa eneo hilo kwa kiasi kikubwa ‘’ alisema Jaji Mkuu.
Serikali
na viongozi mbalimbali wamekuwa wakirejea misingi ya kimataifa ya haki za
binadamu kwenye matamko ya sera na hotuba mbalimbali. Mahakama inatambua kuwa,
uhuru wa vyombo vya habari ni nguzo muhimu ya kupambana na ukiukwaji wa haki za
binadamu, kukuza utawala bora pamoja na kukuza demokrasia. Alitoa mfano wa
uhuru wa wa vyombo vya habari kati ya India na China, ambazo zote zilipata uhuru
kwa wakati mmoja ila china ilifanya vizuri katika maendeleo ya kijamii na uchumi lakini katika eneo moja India
iliipiku China. India huru iliweza kuipiku China kwa kushinda majanga mbalimbali
kama njaa .Hiii iliwezekana kwa sababu ya mfumo wa vyama vingi na uhuru wa
vyombo vya habari. Vyombo huru vya habari huonya jamii juu ya majanga
mbalimbali yanayoweza kutokea, na maonyo hayo hufanya jamii kujikinga mapema. Kwa
maana hiyo, uhaba wa upatikanji wa habari ni aina nyingine ya umasikini na
inaaminika kuwa, kwa kiasi kikubwa bila taarifa sahihi huwezi kufanya maamuzi.
Mahakama ya Tanzania kwa kutambua changamoto
na umuhimu wa utoaji na upatikanaji wa habari kote kwa watumishi wa Mahakama na
waandishi wa habari, ilifanya mambo
kadhaa yakiwemo, kwa kushirikiana na
Baraza la Habari la Tanzania (MCT)
yalianzishwa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari yakilenga namna bora ya
kuripoti habari za Mahakama. Waandishi mbalimbali 42 walinufaika na mafunzo
hayo na matunda yake yameanza kuonekana kwa kufuatilia habari mbalimbali za
Mahakama kwenye vyombo vya habari.
Aidha,ili kuhakikisha kuwa waandishi wetu wa
habari wanapata taarifa za Mahakama ya Tanzania kwa wakati na urahisi,kwa
kushirikiana na Tasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA) yamenzishwa mafunzo maalum
yahusuyo upatikanaji wa taarifa na huduma bora kwa wateja kwa huduma ya kada
mbalimbali za Mahakama. Hadi sasa zaidi ya watumishi 150 wamenufaika na mafunzo
hayo. Kwa hiyo, ni kweli kuwa juhudi hizi zinazofanywa na Mahakama inaendana
kwa kiasi kikubwa na dhima ya mwaka huu ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari
nchini.
Dr. Reginald Mengi, Mwenyekiti wa Wamiliki
wa Vyombo vya Habari Tanzania MOAT (aliyesimama), akisoma risala fupi wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari Duniani kwa 2016.
Hata hivyo, ni kweli
usiofichika kuwa vyombo vya habari vinapaswa kupewa pongezi kubwa kwa kufanikisha mchakato mzima wa uchaguzi
mwaka jana kwa kuripoti habari cha uchaguzi kuanzia wakati wa uchukuaji
fomu,kuteua wagombea na suala zima la kampeni. Vyombo vya habari vilichangia
kwa kiasi kikubwa katika kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi
ule wa kihistoria.
Kuhusu uhuru wa habari na kujieleza,
Mahakama inaamini haki ya msingi ya uhuru kujieleza, ukihusisha uhuru wa vyombo
vya habari na haki ya kupata taarifa kama katiba inavyosema. Lakini kwa upande
mwingine, Mahakama haiamini katika kusema chochote bila kujali unakisemea
wapi,kwa nani na kwa manufaa gani. Hivyo Mahakama inamini kuwa haki yoyote
lazima iambatane na wajibu na pia inaamini kuwa uwepo wa sheria nzuri ya vyombo
vya habari ni chachu kubwa ya maendeleo. Hata hivyo, sheria hizo nzuri haziwezi
kupatikina bila kushirikisha wadau husika. Mahakama inaaminini kuwa wote
wanaohusika katika kutunga sheria mbalimbali watashirikiana kufanya kazi hiyo
sio kwa maslahi ya mtu fulani bali kwa maslahi ya nchi.
Tunaamini kuwa jukumu
la msingi la vyombo vya habari ni kusimamia uwajibikaji na utawala bora na kuwa
chachu ya maendeleo ya nchi. Aidha, ni wazi kuwa utekelezaji wa jukumu hili kwa
vyombo vya habari hauwezekani kama hakuna sheria huru na endelevu ya vyombo vya
habari. Hivyo Mahakama ina nia ya dhati kabisa kushirikiana na vyombo vya
habari ikiwa kila mtu mhusika atatekeleza wajibu wake ili kuleta Tanzania yenye
mafanikio.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa
katika katika Maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yaliyofanyika Kitaifa katika
Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati
wa kuripoti masuala ya uchaguzi kwa
kiasi kikubwa hata katika demokrasia
iliyokomaa popote pale, bado kuna tabia ya vyombo vya habari kuonesha mapenzi
binafsi na vyama au mgombea fulani na vyombo vya habari huendeleza malumbano
baina ya chama fulani na wafuasi wao na kusahau mambo ya msingi ya maendeleo
wananchi. Ni tabia ya baadhi ya vyombo vya habari kuendeleza kejeli ,kashfa na
matusi na kuona ni kawaida katika jamii.’’Mambo haya yameonekana hapa kwetu
kwenye uchaguzi wa mwaka jana’’ alisisitiza Jaji Mkuu.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mnauye (wa tatu toka kulia walioketi) katika picha
ya pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa ,Wanahabari na Wadau wa Habari
wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016,yaliyofanyika mkoani Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni