Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (katikati) akielezea jambo mbele ya viongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) picha ya chini, alipokuwa katika Mkutano uliofanyika kati ya Viongozi wa Mahakama na Mawakili, katika Mkutano huo uliofanyika mapema Julai, 27, 2016 katika Ukumbi wa Maktaba, Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Mhe. Jaji Mkuu amesisitiza kuimarisha ushirikiano baina ya pande hizo mbili kwani kazi ya utoaji haki inategemea ushirikiano wa wadau ikiwa ni pamoja na Mawakili. kulia kwa Mhe. Jaji Mkuu ni Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kushoto kwa Mhe. Jaji Mkuu ni Mhe. Jaji Mzuna, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Pamoja na hayo, Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kuwa ili kuweza kuendelea kutoa huduma iliyo bora kwa wananchi, Majaji, Mahakimu pamoja na Mawakili wote kwa pamoja wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata misingi na taratibu za sheria zilizopo.
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta (aliyesimama) akieleza jambo mbele ya Mkutano kati ya Uongozi wa Mahakama pamoja na Mawakili uliofanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani (T).
Wajumbe wa Mkutano huo wakiendelea na majadiliano.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (aliyeketi katikati), Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (wa tatu kushoto), Mhe. Jaji Mzuna, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam (wa pili kulia), Wakili Msomi, Bw. John Seka, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (wa tatu kulia) pamoja na wajumbe wengine wa Uongozi wa TLS walioketi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha mkutano wao uliofanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani (T).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni