Alhamisi, 28 Julai 2016

MAFUNZO YA MPANGO MKAKATI WA MAHAKAMA YAENDELEA KUTOLEWA KATIKA KANDA MBALIMBALI ZA MAHAKAMA NCHINI

Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro, Bw. Nestory Mujunangoma (aliyesimama) akitoa somo kwa Watumishi wa Mahakama kanda hiyo juu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania, katika mafunzo hayo ya utoaji elimu wa Mkakati huo wa Mahakama watumishi wanajulishwa juu ya mikakati mbalimbali iliyoweka katika Mpango huo, yote ikiwa inalenga katika kuboresha huduma ya utoaji haki haki nchini.
Mtendaji akiendelea kutoa somo
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe akitoa somo juu ya Mpango Mkakati wa Mahakama kwa watumishi wa Mahakama ya Mkoa Njombe (hawapo pichani).
Mtendaji wa Mahakama, Kanda ya Njombe, Bi. Maria Francis Itala, akitoa somo la Mpango Mkakati kwa Watumishi wa Mahakama hiyo
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Njombe wakiwa katika Mafunzo maalum ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) yanayoendelea kutolewa na Wasajili, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mbalimbali za Mahakama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni