Msajili Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati akizungumza na Watumishi wa
Mahakama waliokuwa wakihudhuria Mafunzo kuhusu Uandaaji na Utekelezaji
wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania leo mjini Dodoma. Mheshimiwa
Revokati aliwashukuru watumishi hao kwa kuwa watiifu katika Mafunzo hayo
na kuwataka kutumia ujuzi walioupata kutekeleza majukumu yao kika,ilifu
ili wananchi waweze kupata haki kwa wakati. Mafunzo hayo yalihudhuriwa
na watumishi zaidi ya 132 wa Mahakama wakiwemo Mahakimu Wafawidhi wa
Mikoa na Wilaya, Wasajili, Manaibu Wasajili, Wajumbe wa kikao cha Menejimenti kutoka Makao Makuu pamoja na Watendaji wa Mahakama kutoka mikoa yote nchini.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mafunzo ya siku kumi kuhusu uandaaji na Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania mjini Dodoma leo
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa darasani kwa siku yao ya mwisho ya Mafunzo kuhusu Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania leo mjini Dodoma
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama wakimsikiliza Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati (Hayupo Pichani) wakati akifunga Mafunzo kuhusu Uandaaji na Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mhimili huo leo mjini Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni