Jumamosi, 30 Julai 2016

MAFUNZO YA UTOAJI ELIMU YA MPANGO MKAKATI WA MAHAKAMA YA TANZANIA YAENDELEA KUTOLEWA NA MAAFISA MBALIMBALI WA MAHAKAMA NCHINI

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Mhe. Aishieli Sumari akiwa ameshikilia bango lenye namba tofauti kwa kila Mahaama ambazo zimewekwa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kutoa malalamiko yao juu ya huduma za Mahakama hususani masuala ya rushwa. Mabango hayo ambayo yamesambazwa Mahakama zote ni moja ya jitihada za kuboresha huduma ya utoaji haki nchini kwa kupata mrejesho kutoka kwa wananchi. wa pili kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Mhe. Benedict Mwingwa, wa pili kulia ni Mhe. Zahra Maruma, Naibu Msajili, Mahakama ya Rufani (T) aliyepo Kanda ya Moshi kwa kazi ya kutoa elimu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania, wa kwanza kushoto ni Mhe. Mpepo, Msajili wa Kanda ya Moshi.
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Moshi, Bw. Donald Festo Makawia, akiwapo somo Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Moshi, Mpango Mkakati huo una lengo la kubadili taswira ya Mahakama hususani kuboresha kazi kuu ya Mahakama ambayo ni utoaji wa haki kwa wananchi.
Mkurugenzi Msaidizi-Utawala, Mahakama ya Tanzania, Bi. Wanyenda Kutta (wa kwanza kulia), Bw. Elvin Mwakajinga, Mtendaji-Mahakama Kanda ya Iringa (katikati), na Mhe. Ngunyale, Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa wakiwa wameshikilia Bango la Mahakama lenye namba za simu kwa ajili la kuwawezesha wateja wa Mahakama kutoa maoni na malalamiko yako kwa lengo la kuboresha huduma za Mahakama.

Baadhi ya Watumishi wa Mahakama- Iringa wakiwa katika mafunzo maalum ya Mpango Mkakati yanayoendelea kutolewa katika Mahakama mbalimbali Nchini lengo ni kuwaeleza watumishi kilichomo ndani ya mkakati huo ambao ni wa miaka mitano 2015/2016-2019/2020
Bw. Fidelis Lucas Jalad (aliyesimama), Mtendaji wa Mahakama, Kanda ya Kigoma, akifungua warsha ya mafunzo ya Mpango Mkakati wa Mahakama, walioketi ni Maafisa wa Mahakama wanashiriki katika utoaji elimu wa Mpango Mkakati huo kwa Watumishi wa Mahakama-Kigoma.
Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Kigoma wakisikiliza kwa Makini elimu inayotolewa juu ya Mpango Mkakati wa Mahakama.
Mhe. David Mrango, Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam (kushoto) akimkabidhi bango Bi. Eva Kaduma (Afisa Maalalamiko), Mkoa wa Pwani
Watumishi wa Mahakama, Mkoa wa Pwani, wakiwa katika mafunzo ya Mpango Mkakati wa Mahakama.
Mhe. David Mrango, Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akimkabidhi mabango/vipeperushi mbalimbali RAS wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Zuberi Samataba kwa ajili ya kubandikwa katika Wilaya za Mkoa wa Pwani ili wananchi waweze kupiga simu za malalamiko yanayohusu vitendo vya rushwa na tabia zisizofaa Mahakamani, Kushoto ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani, Evarist Mmbagga.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Evarist Ndikiro (wa pili kulia), Mhe. David Mrango, Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam (wa pili kushoto), Bw. Evarist Mmbagga, Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani (wa kwanza kulia) na Mhe.Elisabeth Nyembele (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumtembelea Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kumueleza juu ya Mpango Mkakati wa Mahakama na kupata maoni yake kuhusu mkakati huo.
Miongoni mwa Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Kilosa wakiwa katika mafunzo maalum ya Mpango Mkakati yanayoendelea kutolewa na Maofisa mbalimbali wa Mahakama, lengo ni kuwapa uelewa watumishi na wadau wa Mahakama juu ya Mkakati huo wenye lengo kubwa la kubadili taswira ya Mahakama ya Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni