Jumatatu, 1 Agosti 2016

JAJI KIONGOZI MAHAKAMA KUU YA TANZANIA ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA KIBAHA NA NYUMBA ZA MAHAKIMU BAGAMOYO MKOANI PWANI

Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali mapema afanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha na nyumba za Mahakimu, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo fupi aliyoambatana na Mtendaji, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mtendaji Kanda ya Dar es Salaam, pamoja na Waandishi-Ujenzi, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Jaji Kiongozi amesifu teknolojia inayotumika katika mradi huo wa Moladi na kuongeza kuwa mradi huo unaweza kwa kiasi kikubwa kuwa mkombozi katika kukabiliana na changamoto ya miundombinu ya Mahakama.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Wilaya Kibaha, lililopo katika ujenzi chini ya teknolojia ya Moladi, kwa sasa jengo hilo lipo katika hatua ya upauaji.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (mwenye koti la kijivu) akiongea jambo alipokuwa katika kiwanja cha Mahakama kilichopo eneo liitwalo Ukuni lililopo Wilayani Bagamoyo, ambao kuna mradi wa ujenzi wa nyumba mbili (2) za Mahakimu, kwa sasa ujenzi huo upo katika hatua za awali (msingi). Waliosimama pamoja na Mhe. Jaji Kiongozi ni Mtendaji,  Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sollanus Nyimbi, (wa kwanza kulia), Bi. Mary Shirima, Mtendaji, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam (mwenye fulana ya bluu bahari) na Waandisi wa Mahakama (wawili waliosimama katikati) na baadhi ya Maafisa wengine wa Mahakama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni