Jumanne, 2 Agosti 2016

MAAFISA MBALIMBALI WA MAHAKAMA WAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MPANGO MKAKATI WA MAHAKAMA KWA WATUMISHI WAKE

Mhe. John Mgeta, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga,  Mhe. Romulus Mbuya, Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, (wa kwanza aliyeketi kwa mbele upande wa kulia), Bi. Hellen Mkumbwa, Kaimu Mtendaji, Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi (katikati), Bw. Geofrey Mashafi, Mchumi Mwandamizi, Mahakama ya Tanzania (wa kw anza kulia) pamoja na Maafisa wengine wa Mahakama wakiwa ofisini kwa Mhe. Jaji Mfawidhi huyo kumueleza kwa ufupi kuhusu Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania.
Mhe. Romulus Mbuya, Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga akimkabidhi simu kwa ajili ya kupokea malalamiko Bw. Albinus Mgonya, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa (aliyesimama katikati kwa mbele), aliyesimama wa kwanza kulia ni Bi. Hellen Mkumbwa, Kaimu Mtendaji, Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi. Vifaa mbalimbali vinasambazwa katika Mahakama pamoja na Ofisi za Wakuu wa Mikoa lengo likiwa ni kuwafikia wananchi na kuwapa fursa ya kutuma maoni yao na malalamiko ili kuweza kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.
Uongozi wa Mkoa wa Rukwa wakiwa wameshikilia bango walilopewa na Uongozi wa Mahakama pindi walipotembelea katika Ofisi hizo za Katibu Tawala lengo likiwa ni kuwapa vifaa mbalimbali vya Mahakama vyenye jumbe mbalimbali za kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa sheria. hususani masuala ya Rushwa, bango hilo lina namba mbalimbali za kila mkoa ambazo zinamuwezesha Mwananchi kutuma maoni au malalamiko kuhusu huduma za Mahakama.
 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, Mhe. John Mgeta (aliyesimama) akifungua mafunzo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania. (kushoto) ni Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Mhe. R. Mbuya, wa pili kushoto ni Bw. Emmanuel Munda, Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga, Bi. Hellen Mkumbwa, Kaimu Mtendaji-Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi. kulia ni Wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Sumbawanga wakiwa katika Mafunzo ya Mpango Mkakati yaliyofunguliwa rasmi na Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo, Mhe. John Mgeta.
Bw. Samson Mashalla, Mtendaji, Mahakama Kuu-Masjala Kuu, (aliyesimama), akitoa somo la Mpango Mkakati kwa Watumishi wa Mahakama Kanda ya Lindi, mapema wiki hii. Maafisa.
Baadi ya Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Lindi wakiwa katika mafunzo ya Mpango Mkakati wa Mahakama.
Bw. Samson Mashalla, Mtendaji, Mahakama Kuu-Masjala Kuu (kushoto) akimkabidhi kitabu cha muongozo wa malalamiko Mhe. Lilian Rugarabamu, akipokea kwa niaba ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi  Lindi 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni