Jumanne, 19 Julai 2016

MAHAKAMA YA RUFANI- TANZANIA YAANZA VIKAO VYAKE 'COURT SESSION' MTWARA

Mahakama ya Rufani (T), imeanza vikao vyake vya kusikiliza kesi mapema tar 18.07.2016 mkoani Mtwara.

Kwa mujibu wa Naibu Msajili, Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Elizabeth Mkwizu jumla ya Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani wapo mkoani humo kwa ajili ya kazi hiyo.

Mhe. Mkwizu alisema kuwa, katika vikao hivyo jumla ya mashauri 25 yatasikilizwa na kuongeza kazi hiyo itafanyika na kukamilika ndani ya wiki tatu.

Wahe. Majaji wa Mahakama wakiwa katika gwaride maalum la ufunguzi wa kikao cha Mahakama ya Rufani kilichoanza rasmi mkoani humo, alisimama kwa juu ni Mhe. Nathalia Kimario, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Semistocles Kaijage (aliyesimama kwa chini aliyepo katikati), kushoto kwa Mhe. Kaijage ni Mhe. Shaban Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Kulia ni Mhe. Fauz Twaib, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Maaskari wakiwa katika gwaride la ufunguzi rasmi wa vikao vya Mahakama ya Rufani katika eneo la Mahakama Kuu, Mkoani Mtwara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni