Jumatano, 20 Julai 2016

MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA AKUTANA NA MAJAJI WASTAAFU WA MAHAKAMA YA TANZANIA

Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (wa pili kushoto) akisisitiza jambo katika Mkutano pamoja na Wahe. Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Tanzania walipokutana mapema leo. Aliyeketi kulia kwa Mhe. Jaji Mkuu ni Mhe. Thomas Mihayo, Rais wa Chama cha Majaji Wastaafu, kulia kwa Jaji Mihayo ni, Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Katika Mkutano huo masuala kadhaa yenye lengo la kuboresho ustawi wa Mahakama yalijadiliwa.

Mhe. Jaji Mkuu akiendelea kuongea na Wahe. Majaji Wastaafu

Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (aliyesimama) akielezea kitu mbele ya Wahe. Majaji wastaafu waliohudhuria katika kikao hicho.

Mhe. Thomas Mihayo, Rais wa Chama cha Majaji Wastaafu nchini (aliyesimama) akieleza jambo katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na Wahe.Majaji wastaafu, kama Mhe. Jaji Lubuva, Mhe. Jaji Kissanga,Mhe. Jaji Salome Kaganda, Mhe. Jaji Msumi, Mhe. Jaji Manento, Mhe. Jaji Mrosso,Mhe. Jaji Jundu na Wahe. Majaji wastaafu wengineo. Viongozi wa Mahakama waliokuwepo katika mkutano huo ni Mhe. Jaji Mkuu, Mhe. Jaji Kiongozi pamoja na Mhe. Mtendaji Mkuu.
Miongoni mwa mambo yalijadiliwa ni pamoja na kuendeleza ushirikiano wa kiutendaji ili kuendelea kuboresha huduma za Mahakama, maadili ya kiutendaji n.k.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni