Mhe. Jaji Mkuu akisaini kitabu cha wageni alipowasili Mahakama ya Wilaya Siha
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Moshi alipowasili Mahakama Kuu mapema tar. 14.07.2016 kwa ziara ya kikazi katika Kanda hiyo.
Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu amepata nafasi ya kuzindua rasmi Mahakama ya Mwanzo Bomang'ombe-Moshi kama inavyoonekana katika picha
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akiwa amekata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mahakama ya Mwanzo Bomang'ombe Wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro, upatikanaji wa jengo hilo la Mahakama ya Mwanzo utarahisisha upatikanaji wa huduma ya haki kwa wananchi wa eneo hilo ambao kwa muda mrefu walikuwa wakihangaika. Lengo la Mahakama ya Tanzania ni kusogeza huduma ya Mahakama katika ngazi ya Kata ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa kila mwananchi.Mhe. Jaji pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama wakielekea eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kupanda mti wa kumbukumbu uliopandwa na Mhe. Jaji Mkuu katika Mahakama hiyo.
Mhe. Jaji Mkuu akipanda mti wa kumbukumbu ndani ya eneo la Mahakama ya Mwanzo Bomang'ombe aliyoizindua rasmi.
Mhe. Jaji Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mahakama, Kanda ya Moshi kwenye uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo Bomang'ombe-Moshi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni