Jumatano, 24 Agosti 2016

BAADHI YA MAJAJI NA WATUMISHI WENGINE WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAUAGA MWILI WA JAJI MSTAAFU RWAKIBARILA.


Jaji wa Mahakama  Rufani, Mheshimiwa  Shaban Ally Lila akiuaga  mwili wa  Marehemu  Jaji Gabriel Kamugisha Rwakibarila(Mheshimiwa Jaji Mstaafu)  kwenye ibada ya kuuaga mwili huo iliyofanyika jana kwenye Kanisa  Katoliki la Mtakatifu Theresia, ambalo marehemu alikuwa  akisali na akishirikiana  waumini wenzake katika shughuli mbalimbali,lililopo  Kimara –Temboni jijini Dares Salaam.




    Jaji Kiongozi, Mhe. Ferdinand  Wambali (wa kwanza kushoto)akipeana mkono na Mhe. Shaban Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani (wa pili kushoto), wa kwanza kulia ni Mhe. Mussa Kipenka, Jaji wa Mahakama ya Rufani, wa pili kulia ni Mhe. Richard Mziray, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Waheshimiwa Majaji hao pamoja na wengine walikuwa msibani kwenye hafla ya kuuaga mwili wa Mhe. Gabriel Rwakibarila, Jaji Mstaafu-Mahakama Kuu ya Tanzania, ibada hiyo ilifanyika jana nyumbani kwa marehemu, Kimara –Temboni jijini Dar es Salaam.
 
   Baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika ibada hiyo iliyofanyika jana kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Theresia ambalo marehemu alikuwa akisali na kushirikiana na waumini wenzake katika shughuli mbalimbali,lililopo Kimara –Temboni jijini Dares Salaam.Marehemu  alifariki dunia tarehe 16.08.2016,ulisafirishwa jana na unatarajiwa kuzikwa leo mkoani Kagera.



    Rais wa Chama cha Majaji Wastaafu, Mheshimiwa Thomas Mihayo  akisaini kitabu cha maombolezo  mara baada ya kufanyika kwa ibada ya kuuga mwili huo iliyofanyika jana nyumbani kwa marehemu,Kimara –Temboni jijini Dares Salaam.Mwili wa Jaji Gabriel  Kamugisha Rwakibarila.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni