Jumanne, 20 Septemba 2016

JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI (T), MHE. ENGERA KILEO AAGWA RASMI KITAALUMA BAADA YA KUSTAAFU


Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Engera Kileo akitoa neno la shukrani mbele ya baadhi ya Majaji wa Mahakama pamoja na wageni waalikwa  (hawapo pichani) walioshiriki katika hafla fupi ya kumuaga kitaaluma iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam, Mhe. Jaji Kileo amemaliza muda wake wa kazi baada ya kutumikia Mahakama kwa kipindi cha miaka 40. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, kulia ni Mhe. Bernard Luanda, Jaji wa Mahakama ya Rufani (T).

Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani walipokuwa katika hafla fupi ya kumuaga Kitaaluma, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Engera Kileo (wa tatu kulia) aliyemaliza muda wake katika utumishi wa Mahakama, wa kwanza kulia ni Mhe. Sauda Mjasiri, Jaji wa Mahakama ya Rufani , wa pili kulia ni Mhe. Bernard Luanda, Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama pamoja na wageni wengine wakiwa katika hafla hiyo
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani walioshiriki kumuaga Kitaaluma Jaji mwenzao, Mhe. Engera Kileo, baada ya kustaafu (wa tatu kulia), katika neno lake la shukrani, Mhe. Kileo amewataka Majaji wenzake kutoa haki kwa wananchi bila upendeleo kwa kuangalia haki ya msingi kuliko ufundi wa kisheria. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, (wa tatu kushoto), pamoja na Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe.Engera Kileo (wa tatu kulia), waliosimama nyuma ni baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioshiriki katika hafla hiyo fupi.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni