Muonekano wa jengo la Mahakama ya Wilaya Mkuranga
lililopo katika ujenzi, jengo hili linajengwa kwa kutumia teknolojia
ijulikanayo kama Moladi.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa
Mahakama ya Wilaya Mkuranga mkoani Pwani.
Mhandisi, Mahakama ya Tanzania, Bw. Coelestine
Rutasindana akionesha kitu katika jengo hilo, Mhandisi huyo pamoja na
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Mwangu (wa
kwanza kushoto) na Mhandisi-Ujenzi, Mahakama, Bw. Khamadu Kitunzi (aliyeshika
kitabu) walitembelea katika Mahakama hiyo mapema tar 30.09.2016, kujionea
maendeleo ya ujenzi huo ambao umefikia katika hatua ya upauaji.
Mkurugenzi wa Fedha Mipango na Ufuatiliaji,
Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Mwangu (kushoto) pamoja na Mhandisi-Ujenzi, Mahakama,
Bw. Khamadu Kitunzi wakikagua jengo la
Mahakama ya Wilaya Mkuranga lililopo katika ujenzi.
Mhandisi-Ujenzi Mahakama akitoa akifafanua jambo
kwa Msimamizi wa Mradi wa Moladi, Bw. Abeid, ( wa kwanza kulia) walipotembelea
mradi huo kujionea hatua iliyofikiwa. Ujenzi na urekebishaji wa Mahakama
mbalimbali nchini ni moja ya jitihada/maboresho yanayofanywa na Mahakama ya
Tanzania katika kuhakikisha kuwa huduma ya utoaji haki inawafikia wananchi
wote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni