Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo
akizungumza na Jaji Mkuu alipofika ofisini kwake leo kumkabidhi Bendara ya
Taifa pamoja na Bendera ya Afrika Mashariki.
Jaji Mkuu wa
Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendara ya Taifa na Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo ofisini kwake leo jijini Dar salaam.
Jaji Mkuu wa
Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendara ya Afrika Mashariki na Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo ofisini kwake leo jijini Dar salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed
Chande Othman akiifurahia zawadi ya Tai ya Bendera ya Taifa aliyokabidhiwa na Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo ofisini kwake leo jijini Dar salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kabla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo ofisini kwake leo jijini Dar salaam.
Jaji Mkuu wa
Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akimwonyesha Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali, Kassian Chibogoyo kitabu cha Sheria kuhusu matumizi ya vielelezo vya Taifa ofisini
kwake leo jijini Dar salaam wakati alipokuwa akikabidhiwa
Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki.
MPIGA
CHAPA MKUU WA SERIKALI AMKABIDHI MHE. JAJI MKUU BENDERA YA TAIFA NA YA AFRIKA
MASHARIKI
Na
Mary Gwera, MAHAKAMA
JAJI Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Mohamed Chande Othman amezitaka Wizara, Halmashauri na Taasisi nyingine za
Serikali kutumia vielelezo vya Taifa kama bendera na nembo ya taifa katika
ofisi zao ili kuenzi tunu na vielelezo vya Taifa.
Aliyasema hayo ofisini
kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea rasmi bendera
ya Taifa na Afrika Mashariki kutoka kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian
Chibogoyo.
Alisema kuwa vielelezo hivi vya taifa vinalindwa kisheria
kwa hiyo inabidi vipate heshima yake kwa kuwa vinawakilisha taifa.
“Sheria pia inavitambua
vielelezo hivi hivyo ni muhimu vikapewa heshima yake, kwani hata mtu akichezea
vitu hivi anaweza kufungwa kwa mujibu ya sheria,” alisisitiza Jaji Mkuu.
Aliongeza pia Mahakama
ya Tanzania pia iko katika mchakato wa kupata bendera yake kama ilivyo kwa
Taasisi nyingine kama Bunge, pamoja na nembo yake ili ziweze kutumika katika
Mahakam azote nchini.
Awali; akiongea na Jaji
Mkuu pamoja na waandishi wa habari kabla ya makabidhiano hayo, Mpiga Chapa Mkuu
wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo pia alizitaka Taasisi za Serikali kutopuuzia
umuhimu wa matumizi wa vielelezo vya Taifa.
Alisema kuwa baadhi ya
Ofisi nyeti za Serikali hazina bendera na vielelezo vingine muhimu ambavyo
vinaiwakilisha Taifa na kusisitiza matumizi yake ili kuenzi tunu za Taifa.
“Ofisi nyingi za
Serikali zinatumia bendera zilizochakaa na nyingine hazina kabisa, vitu hivi ni
muhimu kwa taifa hivyo ni vyema kuvienzi na kuvithamini pamoja na kuvitunza,”
alisema Bw. Chibogoyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni