Jumatatu, 14 Novemba 2016

JAJI KIONGOZI MAHAKAMA KUU YA TANZANIA ATEMBELEA MAHAKAMA KUU BUKOBA, AMPA POLE MKUU WA MKOA WA KAGERA KUFUATIA TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (wa pili kushoto) akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Mhe. Salum Kijuu pindi alipomtembelea ofisini kwake kumpa pole kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mnamo tarehe 10.09.2016 na kusababisha maafa katika baadhi ya miundombinu mkoani huo, Mahakama Kuu ikiwa moja wapo. Kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu- Kanda ya Bukoba, wa kwanza kushoto ni Mhe. Ilvin Mugeta, Msajili- Mahakama Kuu ya Tanzania.
     Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, (wa pili kulia) akikagua jengo la Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba ambalo lilipata mipasuko ‘minor cracks’ kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Pamoja ni Jaji Kiongozi, wa pili kushoto ni Mhe. Jaji Matogoro, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, wa nne kushoto ni Mhe. Ilvin Mugeta, Msajili- Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye aliambatana na Mhe. Jaji Kiongozi katika ziara yake Mkoani humo.
    Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Salvatory Bongole, akiongea kitu mbele ya Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Bukoba kabla ya kumkaribisha rasmi Mhe. Jaji Kiongozi kuongea na Watumishi wa Mahakama wa Kanda hiyo mara baada ya kukagua jengo la Mahakama lililopata maafa kufuatia tetemeko la ardhi.
   Baadhi ya Watumishi wa Mahakama- Kanda ya Bukoba wakimsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi (hayupo pichani) walipokuwa katika Mkutano na Mhe. Jaji Kiongozi, katika Mkutano huo Mhe. Jaji Kiongozi amewaasa Watumishi wote wa Mahakama kufanya kazi kwa kujituma kwa manufaa ya wananchi ambao ndio wateja wa Mahakama, alisema kuwa wananchi hawaangalii mavazi wala kitu kingine, wanachohitaji ni huduma bora, ikiwemo upatikanaji wa hukumu zao kwa wakati.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni