Na
Lydia Churi, Mahakama
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa
Ferdinand Wambali amesema Mahakama ya Tanzania itamuenzi aliyekuwa Spika Mstaafu wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta kwa kuendelea kufanyia kazi mchango
wake wa mawazo alioutoa enzi za uhai wake katika uendeshaji wa shughuli za Mahakama nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Spika huyo Mstaafu leo katika viwanja vya Karimjee jijini
Dar es salaam, Jaji kiongozi alimwelezea Marehemu Sitta kuwa ni mtu aliyekuwa akitoa maoni mbalimbali kuhusu masuala ya haki na sheria nchini kwa Mahakama katika kipindi
cha uhai wake.
Alisema Marehemu Sitta alikuwa ni mtu mnyenyekevu na jasiri katika kutoa maoni ya kile alichokiamini ambapo maoni hayo yalikuwa na mchango mkubwa katika uendeshaji wa shughuli za Mahakama.
Jaji kiongozi alitoa pole kwa familia ya marehemu Sitta,
Viongozi wa Serikali na Chama pamoja na watanzania wote kwa kuondokewa na mtu ambaye mchango
wake ulikuwa bado ukihitajika katika maendeleo ya nchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli kuangalia uwezekano wa kutenga eneo maalum mjini Dodoma
kwa ajili ya kuwazikia viongozi na watu wote waliotoa mchango mkubwa katika kuliendeleza taifa
la Tanzania ili iwe ni kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
Aliendelea kushauri kuwa endapo ombi hilo litakubaliwa na Mheshimi wa Rais,
anapendekeza kuwa kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere nalo lihamishiwe kwenye eneo hilo maalum litakalokuwa kwenye Makao Makuu ya nchi mjini
Dodoma.
Ibada kuuga mwili wa Spika Mstaafu iliyoongozwa na Msaidizi wa Askofu wa
KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mchungaji Chediel Lwiza ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,
Chama na madhehebu mbalimbali ya dini.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni pamoja na Rais Magufuli,
Marais wastaafu Benjamen William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais,
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mawaziri wakuu wastaafu na viongozi wengine.
Spika Mstaafu Samwel John Sitta alifariki dunia Novemba 7
mwaka huu nchini Ujerumani alikokwenda kwa ajili ya Matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa Saratani.
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU SPIKA MSTAAFU SAMWEL SITTA
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kul;ia) wakati wa shughuli ya Kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa katika Ibada ya Kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta leo katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na kulia ni Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali akiwa katika Ibada ya Kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta leo katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es salaam. wanaofuatia ni aliyekuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya awamu ya nne Dkt. Mohamed Gharib Billal, Rais wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali akitoa Salaam za Mahakama ya Tanzania kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania katika Ibada ya Kuuaga
mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta leo katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es salaam.
Askari wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta leo mara baada ya mwili huo kuwasili katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es salaam kwa Ibada na Heshima za Mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni mjini Dodoma na baadaye Urambo Tabora kwa Mazishi yatakayofanyika kesho.Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali akiwa katika Ibada ya Kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. wanaofuatia ni aliyekuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya awamu ya nne Dkt. Mohamed Gharib Billal, na Rais wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiwa katika Ibada ya Kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Samwel John Sitta leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. Wanaofuatia ni Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mjane wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo mama Magreth Simwanza Sitta (katikati) akiwa katika Ibada ya Kuuga mwili wa Marehemu mume wake Marehemu Samwel Sitta leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Angela Kairuki akisoma Salaam za Serikali wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu Samwel Sitta
Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye Ibada ya Kuuaga mwili wa Marehemu Samwel Sitta leo jijini Dar es salaam
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mchungaji Chediel Lwiza akihubiri wakati wa Ibada ya Kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni