Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Methew Mwaimu (wa tatu kulia)
mara baada ya kuagwa rasmi kitaaluma mara baada ya kustaafu rasmi Utumishi wa
Mahakama. Hafla hiyo fupi ya kumuaga rasmi iliongozwa na Mhe. Jaji Kiongozi
katika moja ya Kumbi za Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mapema tarehe. 31.10.2016. Walioketi katika picha ni baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu, walioshiriki katika hafla hiyo, wa kwanza kulia ni Mhe. Jaji Msoffe, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T) ambaye pia alishiriki katika hafla hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama pamoja na wadau wengine wa Mahakama wakiwa katika hafla hiyo.
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Methew Mwaimu (wa pili kulia) akitoa neno la shukrani kwa Wahe. Majaji, watumishi pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) walioshiriki katika hafla ya kuagwa kwake kitaaluma iliyofanyika Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha. wa tatu kulia ni Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye aliongoza shughuli hiyo. Walioketi katika meza Kuu ni baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu walioshiriki katika hafla hiyo.
Meza Kuu ikiwa na pamoja na Jaji Mstaafu, Mhe. Methew Mwaimu (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni