Mkuu wa TAKUKURU Mkoa
wa Simiyu, Bw. Asili Elinipenda Mtera akifafanua jambo katika Mkutano baina ya
TAKUKURU na Watumishi wa Mahakama mkoani Simiyu (hawapo pichani) juu ya vitendo vya rushwa, katika mkutano huu
Mkuu huyo alieleza kuwa katika kipindi cha Julai hadi Oktoba mwaka huu, mkoa wa
Simiyu Ofisi za TAKUKURU walipokea jumla ya malalamiko 17 yanayohusiana na Mahakama.
Pichani ni baadhi ya Watumishi wa Mahakama mkoani Simiyu wakiwa katika Mkutano huo, ambapo waliaswa kufanya kwa maadili na kutojihusisha na vitendo vinavyokwenda kinyume na taratibu za Kimahakama.
Mhe. John Francis Nkwabi, Hakimu Mkazi Mwandamizi,Mfawidhi- Mahakama ya Mkoa, Simiyu akifafanua jambo wakati wa Mkutano huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni