Jumatatu, 19 Desemba 2016

JAJI KIONGOZI, MAHAKAMA KUU YA TANZANIA AFUNGA MAFUNZO YA KUBADILISHANA UZOEFU JUU YA UENDESHAJI WA MASHAURI YA JINAI, AWAPA VYETI MAJAJI WALIOSHIRIKI MAFUNZO HAYO

Na, Mary Gwera

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, ametoa wito kwa Majaji nchini kuendelea kutekeleza jukumu lao la kutoa  haki kwa wananchi wote bila upendeleo.

Alisema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya Kubadilishana uzoefu kwa Wahe. Majaji yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hazina, Mkoani Dodoma akisisitiza juu ya utekelezaji wa jukumu la utoaji haki nchini kwa kutoa haki sawa kwa wananchi ambao ndio wateja wao wakuu wa Mahakama.

“Natumaini katika mafunzo haya mmejifunza mengi, pamoja na hayo, nasisitiza kila mmoja wetu kufanya kazi kwa kujituma na kutoa haki sawa kwa wananchi kwani ndio wateja wetu wakuu,” alisema Jaji Kiongozi.

Katika Mafunzo hayo ya siku tano yaliyoanza tarehe 13.12 na kumalizika tarehe 17. 12. 2016 yalilenga katika kubadilishana uzoefu juu ya uendeshaji wa Mashauri ya jinai, taratibu na changamoto mbalimbali zinazowakabili na hatimaye kuja na mikakati ya pamoja ya jinsi ya kukabiliana nazo.
 Mhe. Ferdinand Wambali akiongea jambo alipokuwa akifunga rasmi Mafunzo ya kubadilishana uzoefu juu ya Mashauri ya jinai yaliyofanyika kwa siku saba katika Ukumbi wa Mikutano Hazina, Mkoani Dodoma, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Mhe. Mwanaisha Kwariko, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, wa kwanza kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu- Kanda ya Tanga, Mhe. Imani Aboud, mmoja kati ya walioshiriki Mafunzo hayo, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu- Kanda ya Dodoma, Mhe. Mwanaisha Kwariko, mmoja kati ya walioshiriki Mafunzo hayo, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama , Divisheni ya Ardhi mmoja kati ya walioshiriki Mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Gerald Ndika, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama, Divisheni ya Ardhi mmoja kati ya walioshiriki Mafunzo hayo, Mhe. Panterine Kente, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama, Divisheni ya Ardhi mmoja kati ya walioshiriki Mafunzo hayo, Mhe. Lilian Mashaka, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama Kuu- Kanda ya Tabora, Mhe. Leila Mgonya, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama Kuu- Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Wilfred Dyansobera, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama Kuu- Kanda ya Shinyanga, Mhe. Victoria Makani, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama Kuu- Kanda ya Iringa, Mhe. Rehema Kerefu, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama Kuu- Kanda ya Mwanza, Mhe. Issa Maige, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu- Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Rehema Mkuye, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, kulia ni Jaji-Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama -IJA Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji-Mahakama Kuu- Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Mafunzo hayo.
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (kulia) akimpatia cheti Jaji ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama- IJA- Lushoto alishiriki katika mafunzo hayo.
Waheshimiwa Majaji wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wengine wa Mahakama walioshiriki katika uratibu na maandalizi ya mafunzo hayo.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji walioshiriki katika Mafunzo, wa kwanza kulia aliyesimama ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, wa kwanza kushoto aliyesimama ni Msajili- Mahakama Kuu ya Tanzania- Mhe. Ilvin Mugeta.
Wahe. Majaji wakiwa katika picha ya pamoja na Madereva wao waliofanikisha kuwafikisha katika Mafunzo hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni