Ijumaa, 16 Desemba 2016

JAJI MFAWIDHI, MAHAKAMA KUU- DIVISHENI YA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI ATOA MADA JUU YA CHANGAMOTO ZA MIENENDO YA USIKILIZAJI WA MASHAURI YA MAKOSA YA JINAI



         Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, almaarufu kama Mahakama ya Mafisadi, Mhe. Rehema Mkuye, akitoa mada juu ya taratibu za uendeshaji wa Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi katika Divisheni hiyo, wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Panterine Kente, wa pili kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Wilfred Dyansobera, anayefuata ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Mhe. Jaji. Dkt. Paul Kihwelo.
Mhe. Jaji Mkuye akiendelea kutoa mada.
Waheshimiwa Majaji wanaoshiriki katika mafunzo ya kubadilishana Uzoefu juu ya Uendeshaji wa Mashauri ya Jinai wakimsikiliza, Jaji Mfawidhi wa Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Rehema Mkuye. Katika mada hiyo Mhe. Mkuye alielezea juu ya adhabu za Makosa ya Uhujumu uchumi ambazo zimeongezeka kutoka kifungo cha hadi miaka 15 na kuwa kifungo kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30.
Jaji wa Mahakama Kuu- Divisheni ya Ardhi, Mhe. Dkt. Gerald Ndika akichangia kitu katika mafunzo hayo, pembeni yake ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Leila Mgonya.
Majadiliano ya vikundi yakiendelea kuhusiana na mada.
Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Victoria Makani akichangia jambo katika mafunzo hayo yanayoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano- Hazina mjini Dodoma.
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu- Kanda ya Tanga, Mhe. Iman Aboud akichangia mada.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni