Na
Lydia Churi-Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Mohamed Chande Othman amewataka Mawakili nchini kuzingatia Maadili na kufuata
misingi ya haki katika kutekeleza majukumu yao ili kesi ziendeshwe kwa haki,
haraka na kwa wakati ili kuongeza imani ya wananchi kwa Mahakama.
Akizungumza wakati wa
sherehe za kuwapokea na kuwaapisha Mawakili leo katika viwanja vya Karimjee jijini
Dar es salaam, Jaji Mkuu amesema endapo Mawakili watatekeleza wajibu wao kwa
kutenda haki watasaidia kupunguza mlundikano wa kesi zilizopo kwenye Mahakama mbalimbali
nchini kuanzisha zile za Wilaya mpaka mahakama ya Rufani.
Aidha, Jaji Mkuu amewataka
Mawakili kushirikiana Mahakama pamoja na wadau wengine katika kuutekeleza Mpango
Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ambao pamoja na mambo mengine pia
unalenga kupunguza mlundikano wa kesi kwenye mahakama mbalimbali nchini.
Mhe. Othman pia amewashauri
Mawakili walioapishwa leo kujiendeleza kielimu ili waweze kuongeza ujuzi utakaowasaidia
kupambana na changamoto mbalimbali za kitaaluma na kwenda na wakati.
Amewataka Mawakili hao
kusambaa na kufanya kazi mikoani ili na raia walioko huko nao wapate haki badala
ya wengi wao kung’ang’ania kwenye miji mikubwa pekee kama vile Dar es salaam,
Arusha, na Mwanza.
Naye Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Fednand Wambali amesema suala la ushiriki wa dhati
katika utoaji wa haki nchini limesisitizwa kwa Mawakili walioapishwa leo.
Mhe. Wambali pia amewataka
Mawakili hao kuwa waaminifu kwa Mahakama ya Tanzania na kwa wateja wao ambao n iwananchi
wanaotafuta haki zao.Aliongeza kuwa bila ya Mawakili hao kuwa na maadili hawataweza
kufanya kazi.
Naye Mwanasheria Mkuu
wa Serikali Mhe. George Masaju amewataka Mawakili hao wapya kufanya kazi zao kwa
kufuata maadili ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
Alisema kupitia kamati
ya malalamiko, amepokea malalamiko 71 kati ya mwaka 2015 na 2016 yaliyowahusu Mawakili
kukiuka taratibu na misingi ya kazi yao.
Kwa mujibu wa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, baadhi ya malalamiko yalihusu Mawakili kutokuwatetea wateja wao
ipasavyo, kufanya kazi ya uwakili bila ya kulipia kibali, na kutoa siri za wateja
wao.
Jaji Mkuu wa Tanzania amewakubali na kuwaapisha Mawakili wapya 285
na kuifanya Tanzania kuwa na Mawakili zaidi ya 6080.
Sherehe za kuwakubali na kuwaapisha Mawakili hao zimefanyika kwa
mara ya 55 tangu kuanzishwa kwa sherehe hizo mwaka 1986 hapa nchini.
Waheshimiwa Majaji wakiwasili viwanja vya Karimjee kwa ajili ya sherehe ya kuwapokea na kuwakunbali Mawakili.
Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa na baadhi ya Majaji wa Tanzania wakati wa sherehe za kuwakubali na kuwaapisha Mawakili
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) pamoja na Majaji wengine wakipokea salaam ya Kimahakama kutoka kwa Mawakili walioapishwa leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Mawakili wakiapishwa na Jaji Mkuu (hayupo Pichani) leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Mawakili walioapishwa wakitoa salaam ya kimahakama kwa Waheshimiwa Majaji wakati wa sherehe za kuapishwa kwao leo jijini Dar es salaam
Baadhi ya watumishi wa Mahakama pamoja na waalikwa wengine wakiwa katika sherehe ya kuwakubali na kuwaapisha Mawakili leo jijini Dar es salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza wakati wa sherehe ya kuwakubali na kuwaapisha Mawakili leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawakili aliowapokea na kuwaapisha leo jijini Dar es salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawakili aliowapokea na kuwaapisha leo jijini Dar es salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni