Jumamosi, 7 Januari 2017

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA- TAWJA

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA MKUTANO MKUU WA NANE WA TAWJA ULIOFANYIKA LEO JIJINI    DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) kwa ajili ya kuufunga leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na kulia ni Mwenyekiti wa TAWJA ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga Mhe. Iman Abood.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Majaji kabla ya kufungua Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA). Wa kwanza kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akifuatiwa na Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Iman Abood. Kulia kwa Makamu wa Rais ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akifuatiwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Iman Abood (hayupo pichani) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA). Katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu.
 Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Iman Abood akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo jijini Dar es salaam. 

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza wakati wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo jijini Dar es salaam.


  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza wakati wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua  Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA leo jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Iman Abood wakati wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA leo jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Iman Abood akiwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali wakati wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA leo jijini Dar es salaam


 Majaji Wakuu:
Kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu wakiwa kwenye Mkutano wa TAWJA leo jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa TAWJA kwa niaba ya Wanachama wa chama Hicho leo jijini 
Dar es salaam. 

Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mahakama mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa TAWJA leo jijini Dar es salaam. 

 Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa TAWJA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Chama hicho leo jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa TAWJA leo jijini Dar es salaam. Waliosimama wa tatu kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju.
  Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa TAWJA (Majaji) mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Chama hicho leo jijini Dar es salaam.

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (wa pili kushoto), Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (wa kwanza kushoto) pamoja na wanachama wa TAWJA wakisikiliza Mada ikitolewa wakati wa Mkutano wa Nane wa Chama hicho leo jijini Dar es salaam.


Baadhi ya Wanachama wa TAWJA wakifuatilia jambo wakati wa Mkutano wao wa mwaka leo jijini Dar es salaam.
Wanachama wa TAWJA wakifuatilia jambo wakati wa Mkutano wao wa mwaka leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Hakimu Mkazi  wa Mahakama ya Watoto Kisutu Mhe. Devotha Kissoka.




Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza   Majaji wanawake  na Mahakimu  wa Wanawake nchini kuendelea kutoa elimu na ujuzi  juu ya haki  za binadamu ili kuwezesha jamii kuepukana na  vitendo rushwa,ikiwemo rushwa ya ngono  na ukatili wa kijinsia.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu huyo wa Rais  aliyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane  Mkutano wa Nane wa Mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) uliofanyika  jijini Dar es salaam, ambao umehusisha Majaji Wanawake, Mahakimu Wanawake, wakiwemo baadhi Wanaume.

Mkutano huo wenye lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya utoaji haki na hukumu bila ubaguzi. Kauli mbiu ya mkutano huo ni Kuongoza njia kufikia
hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati”

Aliongeza kwamba chama hicho kina wajibu  wa kuhakikisha upatikanaji wa haki  bila ubaguzi , hususan kwa masuala yanayohusu wanawake na watoto ili kuwezesha ustawi wao kwa ujumla na maendeleo ya nchi.
“ Ninakiaagiza Chama  hiki kuendelea kutoa elimu juu ya haki za binadamu katika jamii kwa maafisa wa Mahakama,  watunga sheria na kwa watu  waliathirika na vitendo  vya rushwa  ya ngono na ukatili wa kijinsia kwa kuwa    utoaji wa elimu ndio, utawezesha  upatikanaji wa haki  kwa wakati kwa  jamii inayohitaji ,” alisema Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Aliongeza kwamba chama hicho kina wajibu  wa kuhakikisha upatikanaji wa haki  bila ubaguzi , hususan kwa masuala yanayohusu wanawake na watoto ili kuwezesha ustawi wao kwa ujumla na maendeleo ya nchi.
Aidha Makamu huyo wa Rais amekishukuru Chama cha Majaji Wanawake cha Dunia(IAWJ) kwa michango na msaada wake kwa  TAWJA kwa program ya miaka mitatu ya  ya kupambana na  vitendo vya rushwa ya ngono vinadaiwa kufanywa na baadhi ya watu wenye madaraka.

Alisema   vitendo hivyo vinasababisha baadhi ya wanawake kutopata huduma mbalimbali  zikiwemo za elimu, ajira, haki na huduma nyinginezo.

Makamu wa Rais pia ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  masuala ya wanawake( na wadau wengine wa TAWJA kwa kuunga mkono mapambano ya aina zote za ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni