Mwezeshaji- kutoka Chuo
cha Uongozi wa Mahakama- Lushoto (IJA), Bw. Amos Kinyonyi mwenye shati jeupe
akitoa mada mapema leo juu ya Mapitio ya jumla kuhusu Utunzaji wa kumbukumbu
kwa njia ya kielektroniki ‘An overview of
Electronic Record Keeping Management.’ kwa washiriki wa Mafunzo hayo ya
siku 10 yanayoshirikisha Maafisa TEHAMA na Wasaidizi wa Kumbukumbu 51 kutoka
Kanda mbalimbali za Mahakama nchini.
Baadhi ya Washiriki wa
Mafunzo wakiwa katika majadiliano ya kikundi mara baada ya kupatiwa somo la
Mapitio ya jumla juu ya Utunzaji wa Kumbukumbu kwa njia ya Kielektroniki.
Msaidizi wa Kumbukumbu kutoka Mahakama ya Rufani
(T), Bw. Felician Assunga akichangia jambo katika mafunzo hayo.
Afisa TEHAMA kutoka, Mahakama Kuu, Divisheni ya
Kazi, Bw. Ally Daudi akichangia jambo wakati wa Mafunzo hayo.
Msaidizi wa Kumbukumbu
kutoka Mahakama ya Wilaya Nyamagana- Mwanza, Bi. Evodia Kakwezi akiwasilisha mbele
ya washiriki wenzie (hawapo pichani).
Afisa TEHAMA, Bi.
Stella Matulile akifafanua jambo mbele ya Washiriki wa Mafunzo ya Utunzaji wa
kumbukumbu kwa njia ya Kielektroniki.
Mafunzo haya yaliyoanza
Januari 03, 2017 na yanayotarajiwa kumalizika tarehe. 13.01.2017 ni muendelezo
wa mafunzo kwa Wasaidizi wa kumbukumbu (RMAs) yaliyokwishafanyika mkoani Dodoma
chini ya Mradi wa Mapambano dhidi ya Rushwa ‘STACA,’ ambapo kwa sasa mafunzo
haya yatatilia mkazo juu ya utunzaji wa kisasa wa nyaraka na kumbukumbu za
Mahakama ikiwemo matumizi ya vitendo vya kutumia mfumo wa Kielektroniki katika
kutunza na kushughulikia kumbukumbu hizo kwa ujumla. (Picha na Mary Gwera,
Lushoto)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni