JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA
TAARIFA KWA UMMA
UONGOZI WA MAHAKAMA YA
TANZANIA, UNAPENDA KUWATAARIFU NA KUWAALIKA WANANCHI WOTE KATIKA SIKU YA SHERIA
NCHINI INAYOASHIRIA KUANZA KWA MWAKA MPYA WA SHUGHULI ZA MAHAKAMA .
KATIKA KUADHIMISHA SIKU HIYO,
SIKU YA SHERIA NCHINI ITATANGULIWA NA WIKI YA UTOAJI WA ELIMU YA SHERIA NA
HUDUMA ZA MAHAKAMA KAMA SEHEMU YA MAADHIMISHO HAYO. UTOAJI WA ELIMU UTAFANYIKA NCHI
NZIMA NA KWA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUANZIA
TAREHE 28 JANUARI HADI TAREHE 1 FEBRUARI 2017 KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI MPAKA
SAA 11:00 JIONI.
TAASISI ZITAKAZOKUWEPO NA
KUJUMUIKA NA MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA UTOAJI WA ELIMU NI PAMOJA NA:
·
TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
·
MAHAKAMA KUU ZANZIBAR
·
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (AGC)
·
OFISI YA MKURUGENZI WA MASHITAKA (DPP)
·
MKEMIA MKUU WA SERIKALI
·
CHUO CHA UONGOZI CHA MAHAKAMA (IJA)
·
MKUU WA KITIVO CHA SHERIA, SHULE YA SHERIA UDSM
·
MKUU WA KITIVO CHA SHERIA, CHUO KIKUU HURIA
·
TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO TANZANIA
(THE LAW SCHOOL OF TANZANIA)
·
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
·
TUME YA KUREKEBISHA SHERIA
·
TAASISI ZINAZOTOA ELIMU NA MSAADA WA KISHERIA (LEGAL
AID)
·
TAKUKURU (PCCB)
·
POLISI
·
MAGEREZA
·
MSAJILI, MABARAZA YA ARDHI
·
CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA (TLS)
·
TUME YA KUREKEBISHA SHERIA
·
WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (RITA)
·
CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE (TAWJA)
·
CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE (TAWLA)
·
SEKRETARIETI YA MSAADA WA SHERIA
·
TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)
·
LEGAL AND HUMAN RIGHT CENTRE
·
BIMA YA AFYA YA TAIFA
·
TPSF
KWA WALE WOTE WENYE MAHITAJI YA KUPATA MSAADA/ELIMU WA
KISHERIA, MALALAMIKO YOYOTE, MAONI AU MAPENDEKEZO
YA UBORESHAJI WA UTENDAJI KAZI WA MAHAKAMA WANAKARIBISHWA KUFIKA.
AIDHA YATAFANYIKA MATEMBEZI YA KUADHIMISHA SIKU YA
UTOAJI WA ELIMU YA SHERIA NCHINI. KWA DSM MATEMBEZI HAYO YATAFANYIKA SIKU YA
TAREHE 29 JANUARI, 2017 SAA 12:00 ASUBUHI YATAKAYOANZIA MAHAKAMA YA HAKIMU
MKAZI KISUTU NA KUISHIA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA. MATEMBEZI HAYO YATAONGOZWA NA RAIS MSTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, MHE. ALI HASSAN MWINYI.
KILELE
CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI KITAFANYIKA TAREHE 02.02.2017, KATIKA
VIWANJA VYA MAHAKAMA VILIVYOPO MTAA WA CHIMALA JIJINI DAR ES SALAAM. MGENI
RASMI ATAKUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. JOHN POMBE
JOSEPH MAGUFULI. SHEREHE HIZO ZITAANZA RASMI SAA 03:00 ASUBUHI.
KAULIMBIU YA MWAKA HUU: ‘’UMUHIMU
WA UTOAJI HAKI KWA WAKATI KUWEZESHA UKUAJI UCHUMI’’
WOTE MNAKARIBISHWA
IMETOLEWA NA OFISI YA MTENDAJI MKUU
MAHAKAMA YA TANZANIA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni