Jumamosi, 28 Januari 2017

MAONYESHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI YAANZA RASMI LEO, JANUARI 28, 2017

Afisa kutoka Mahakama ya Rufani (T) aliyesimama ndani ya Banda akiwapatia maelezo juu ya Mahakama ya Rufani, baadhi ya wananchi walipotembelea katika Maonyesho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza rasmi mapema leo, kwa upande wa Dar es Salaam, Maonyesho hayo yanafanyikia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kuanzia Januari 28 hadi Februari 01, 2017. Kilele cha Wiki ya Sheria ambayo ni Siku ya Sheria nchini itakuwa Februari 01, 2017 na Mgeni rasmi atakuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na itafanyikia katika Kiwanja cha Mahakama kilichopo Mtaa wa Chimala jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Maafisa wa Mahakama wakiwa katika mabanda wakisubiri kuhudumia wananchi wanaotembelea katika Maonyesho hayo.
Mahakama Kuu ya Zanzibar ni moja kati ya Washiriki wa Maonyesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa wa Mahakama wakiwa katika Banda la Utawala- Mahakama ya Tanzania.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza, Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani alipokuwa akiwaelezea juu ya Shughuli mbalimbali za Jeshi la Polisi nchini, POLISI ni moja kati ya Wadau wa Mahakama wanaoshiriki katika Maonyesho hayo.
Muonekano wa baadhi ya mabanda.
Banda la Chama cha Majaji Wanawake Nchini pamoja na Banda la TAWLA vikionekana katika picha, hawa pia ni baadhi ya wadau wanaoshiriki katika Maonyesho. Washiriki wengine ni pamoja na Tume ya Utumishi Wa Mahakama, Mahakama Kuu Zanzibar, Ofisi Ya Mwanasheria Mkuu Wa Serikali (AGC), Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP), Mkemia Mkuu Wa Serikali, Chuo Cha Uongozi Cha Mahakama (IJA), Mkuu Wa Kitivo Cha Sheria, Shule Ya Sheria Udsm, Mkuu Wa Kitivo Cha Sheria, Chuo Kikuu Huria, Taasisi Ya Mafunzo Ya Uanasheria Kwa Vitendo, Tanzania (The Law School Of Tanzania), Tume Ya Haki Za Binadamu Na Utawala Bora, Tume Ya Kurekebisha Sheria, Taasisi zinazotoa Elimu Na Msaada Wa Kisheria (Legal Aid), Takukuru (Pccb), TLS n.k    (Picha na Mary Gwera)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni