JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA
TAARIFA KWA UMMA
Mahakama ya
Tanzania kupitia Mpango Mkakati wake wa Miaka Mitano 2015/16 – 2019/20 imepanga
kupanua wigo wa huduma kwa makundi yenye mahahitaji maalum. Katika Mpango huo
Mahakama inatarajia kujenga Kituo cha Pamoja Kitakachoshughulikia masuala ya
Mirathi. Katika Kituo hicho kutakuwa na huduma za Mahakama ya Mwanzo, Mahakama
ya Wilaya na Mahakama Kuu.
Aidha Huduma za
Kibenki pamoja na Huduma za Mafao kutoka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Huduma za
Msaada wa Kisheria, Usajili wa Vizazi na Vifo n.k zitapatikana katika kituo
hicho ili kurahisisha huduma na kupunguza usumbufu kwa walengwa.
Kituo hicho cha
huduma hii kinatarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2019 Mkoani Dar es salaam
katika Wilaya ya Temeke karibu na Kituo cha Polisi Chang’ombe ilipo Mahakama ya
Mwanzo Temeke.
Hii ni taarifa ya
awali kwa umma kuhusu utekelezaji wa mpango huu.
IMETOLEWA NA
MSAJILI
MKUU
MAHAKAMA YA TANZANIA
MAHAKAMA YA TANZANIA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni