Alhamisi, 9 Machi 2017

WATUMISHI WANAWAKE WA MAHAKAMA WASHIRIKI MAANDAMANO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Baadhi ya Wawakilishi wa Watumishi Wanawake  wa Mahakama ya Tanzania wakiwa wamebeba  bango la Mahakama katika Viwanja  vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam , tayari kwa kuanza Maandamano ya  Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama ya Tanzania, Bibi Wanyenda Kutta (Mwenye nguo Nyekundu) akiwa pamoja na Wawakilishi wa Watumishi Wanawake wa Mahakama ya Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika viwanja vya Mwembe Yanga jana jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wanawake wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika viwanja   vya Mwembe Yanga, vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke,   Mhe. Felix   Lihaniva akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika jana katika Viwanja Vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa  ubunifu wa kiwanda cha ujenzi  kutoka (VOET) Maida Waziri akionyesha  furaha   akipongezwa na mwenzake baada ya kuelezea  vitendo  vya   ujasiri  na kujiamini vilivyomsaidia kuwa mshindi katika sekta ya miundombinu ya barabara wakati wa Madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.  Maadhimisho  hayo yalifanyika  jana jijini Dar es Salaam katika  Kiwanja  cha Mwembe  Yanga.

Wawakilishi wa Watumishi Wanawake wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jana katika Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni