Na Mary Gwera
Mahakama
Rais wa Mahakama ya
Afrika ya Haki za Binadamu amemtembelea Kaimu Jaji Mkuu, ambapo amesisitiza juu
ya ushirikiano kati ya Mahakama yake na Mahakama nchini.
Rais huyo wa Mahakama
ya Afrika, Mhe. Jaji Sylvain ORE` alimtembelea Mhe. Kaimu Jaji Mkuu mapema
Machi 1, katika ofisi zake zilizopo Mahakama ya Rufani (T) jijini Dar es Salaam,
ambapo lengo mojawapo la ujio wake ilikuwa ni kumpongeza Mhe. Kaimu Mkuu nchini
kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo.
Aidha mbali na kutoa
pongezi, ujio wake pia umelenga katika kuendeleza mahusiano yaliyokuwepo wakati
wa utawala wa Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman kwani Mahakama mdau
mkubwa katika Mahakama hii.
Mbali na kumtembelea
Kaimu Jaji Mkuu, Rais huyo wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu
alimtembelea pia, Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand
Wambali.
Akitoa maelezo mafupi
kwa niaba ya Kaimu Jaji Mkuu kwa mgeni huyo, Mhe. Wambali alimueleza juu ya
muundo wa Mahakama nchini na jinsi inavyofanya kazi ya utoaji haki nchini.
Aliendelea kuongelea
juu ya maboresho ya utoaji huduma ya haki kwa wananchi kwamba nia ya Mahakama
ni kuwa na huduma ya Mahakama Kuu kila Mkoa ili kuwawezesha wananchi wa kila mkoa
kupata huduma ya haki.
“Nia ya Mahakama ni
kuwa na Mahakama Kuu katika kila mkoa, kwa sasa kuna zaidi ya mikoa 13 ambayo bado
haina Mahakama Kuu, hivyo kwa Mwaka huu wa fedha Mahakama imepanga kuanza
ujenzi wa jumla ya Mahakama Kuu nne, na tutakuwa tukifanya hivi kwa awamu kadri
bajeti itakavyoruhusu,” alieleza Jaji Wambali.
Mbali na kukutana na
Viongozi hao Wakuu wa Mahakama, Rais huyo wa Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu alipata wasaa wa kujionea muonekano wa kumbi za Mahakama ya Rufani na
Mahakama Kuu ya Tanzania.
Rais huyo kutoka nchini
Ivory Coast amechukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Rais wa Mahakama
hiyo, Mhe. Jaji Augustino Ramadhani.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.
Ibrahim Juma (kulia), akimkaribisha Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE`, alipowasili ofisini kwake Mahakama ya Rufani
(T).
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE`, akitia sahihi kitabu cha Wageni alipowasili
ofisini kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania.
Mhe.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania (kulia) akifurahia jambo alipokuwa wakijadili jambo
na mgeni wake.
Afisa Itifaki, Mahakama ya Afrika ya
Haki za Binadamu, Bw. Simba Tamaambele (kushoto) pamoja na Katibu wa Mhe. Kaimu
Jaji Mkuu, Mhe. Elinaza Luvanda wakifuatilia mazungumzo ya Viongozi hao.
Katibu wa Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, Mhe.
Elinaza Luvanda (kulia) akimuonesha kitu Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE` alipotembelea katika Ukumbi namba 1 wa
Mahakama ya Rufani (T).
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya
Tanzania,Mhe. Ferdinand Wambali (kushoto) akijadili jambo na Rais wa Mahakama
ya Afrika ya Haki za Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE` (kulia), pindi Rais huyo
alipowasili ofisini kwa Mhe. Jaji Kiongozi, katikati ni Afisa Itifaki, Mahakama
ya Afrika ya Haki za Binadamu, Bw. Simba Tamaambele.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya
Tanzania,Mhe. Ferdinand Wambali (kushoto) akimuonesha kitu Rais wa Mahakama ya
Afrika ya Haki za Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE` alipokuwa katika Ukumbi
namba 1 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE` akimuonesha kitu Mhe. Jaji Kiongozi ili kupata
ufafanuzi. (Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni