Mwenyekiti
wa Mkutano wa Mashauriano kuhusu uanzishaji
wa Kituo kimoja cha kushughulikia masuala ya mirathi,
ambaye ni Msajili ya Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe. Ilvin Mugeta (kushoto) akizungumza
jambo na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya,Mhe. Atuganile Ngwala(kulia)
wakati
wa akiendesha majadiliano
ya mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya
Kurekebisha Sheria,uliopo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika
tarehe Machi 02, mwaka 2017.
Mwenyekiti
wa Mkutano wa Mashauriano kuhusu uanzishaji
wa Kituo kimoja cha kushughulikia masuala ya mirathi,
ambaye ni Msajili ya Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe. Ilvin Mugeta (kushoto) akizungumza
jambo na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya,Mhe. Atuganile Ngwala(kulia)
wakati
wa akiendesha majadiliano
ya mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya
Kurekebisha Sheria,uliopo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika
tarehe Machi 02, mwaka 2017.
Mwenyekiti wa Mkutano wa Mashauriano kuhusu uanzishaji wa Kituo cha kimoja cha kushughulikia masuala ya mirathi, ambaye ni Msajili ya Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe. Ilvin Mugeta (kushoto) akiendesha mkutano huo. Ngwala wakati wa akiendesha majadiliano ya mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya Kurekebisha Sheria,uliopo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya,Mhe. Atuganile. Mkutano huo umefanyika tarehe Machi 02, mwaka 2017.
Picha ya
Pamoja ya wadau wa Mkutano wa Mashauriano
kuhusu uanzishaji wa Kituo cha
kimoja cha kushughulikia masuala ya mirathi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya
Kurekebisha Sheria,uliopo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika
tarehe Machi 02, mwaka 2017.
Na Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania.
MAHAKAMA ya Tanzania, ina mpango wa kuanzisha Kituo maalum kitakachoshughulikia masuala ya mirathi ili kuweza kusogeza huduma za masuala ya mirathi kwa wananchi, ikiwa ni hatua ya kuwapunguzia
gharama za fedha wanazozitumia na muda
wanaoutumia.
Kutokana na
eneo la mirathi limeonekana kuwa
na changamoto nyingi na hivyo kuhitaji mtazamo wa pekee Mahakama inaanzisha,
Mpango huo ili kuongeza ufanisi
na katika kushughulikia mirathi na mambo ya kifamilia.,
Aidha hatua hiyo,
itasaidia kuwawezesha makundi maalum ambayo wanawake na watoto wakiwemo na wasimamizi wa
mirathi wanaohitaji huduma hiyo kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na
kukuza uchumi wa nchi.
Kauli hiyo ilitolewa
jana na Mwenyekiti wa Mkutano wa Mashauriano kuhusu uanzishaji
Kituo Maalum cha kushughulikia
masuala ya mirathi, ambaye ni Msajili ya Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe.
Ilvin Mugeta kwenye ukumbi wa mikutano
wa Tume ya Kurekebisha Sheria,uliopo Jijini Dar es Salaam.
“Tuna mapango
wa kuanzisha kituo hicho cha huduma
za Mahakama kuhusiana
na masuala ya mirathi,
ambacho kitakuwa na wadau mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania ili kuhakikisha
huduma za mirathi zinatolewa kwa
wakati bila kupoteza muda na gharama,” alisema Mwenyekiti huyo.
Aliongeza kwamba kituo hicho kitaanzishwa katika jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni mradi
wa mfano, lakini baadae vitaanzishwa katika mikoa mingine.
Aidha Mhe.
Mugeta ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, alisema kituo hicho,
kitaanzishwa katika jiji hilo kwa sababu
tatizo hilo, kubwa kwa sababu lina
wakazi wengi.
Aliitaja sababu
ya kuanzishwa kituo hicho, kimetokana
kwamba Mahakama ya Tanzania huwa inapokea maoni 3,000 kila siku kuhusiana na masuala hayo.
“Kituo hicho kitakuwa na huduma za Mahakama za
Mwanzo, Wilaya na Mahakama Kuu, ili kuweza kuondoa vipingamizi katika utoaji wa huduma hizo.
Alisema katika kituo hicho, kinatarajiwa
kuwa na huduma za
utoaji wa vyeti vya kuzaliwa na cheti kifo, huduma za mifuko ya hifadhi ya jamii na kibenki.
Baadhi ya wadau wa mkutano huo, walipendekeza kwamba elimu
zaidi itolewe kuhusiana na masuala ya
mirathi.
Mkutano huo, ambao umeandaliwa na Mahakama ya
Tanzania, umewashirikisha baadhi ya
viongozi wa Mahakama na wadau
mbalimbali ambao ni Chama
cha Wanasheria Wanawake Tanzania,
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ambayo ni (NSSF), (PSPF), Mamlaka
ya Usimamia Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii (SSRA), Chama cha Mawakili
Tanganyika(TLS) na Baraza Kuu la Waislaamu Tanzania(BAKWATA).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni