Watumishi wa Mahakama
hususani Wahasibu na Watendaji wa Mahakama wameaswa kufuata taratibu na sheria
za fedha katika kufanya malipo mbalimbali.
Hayo yalisema na
Mkaguzi wa Ndani- Mahakama, Bi. Augustina Kimati katika kikao cha pamoja kati
yake na Watumishi hao kilichofanyika Machi 24, mwaka huu Kibaha-Pwani.
Mbali na kuwasisitiza
juu ufuataji wa taratibu stahiki za malipo, Bi. Kimati aliwapa Watendaji hao
mbinu mbalimbali za kufuata ili kuepuka hoja zisizo na msingi hasa pale
watakapotembelewa na Wakaguzi wa nje.
Katika kikao hicho, Bi.
Kimati aliwafunda Wahasibu na Watendaji kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Pwani
kufuata taratibu za fedha na
kuwasisitiza juu ya kufuata Sheria ya Manunuzi Serikalini na ‘Public Finance
Act.’
Mkaguzi wa Ndani-Mahakama ya Tanzania, Bi. Augustina Kimati (kulia) akiwa na Naibu Mtendaji Mkoa wa Pwani, Bi. Stumai Hozza (kushoto) wakiwa katika kikao cha Ukaguzi, Kibaha-Pwani.
Watendaji na Wahasibu wa Mahakama ya Wilaya na Mkoa wa Pwani wakiwa katika kikao cha Ukaguzi kilichofanyika Kibaha Mkoani Pwani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni