Jumamosi, 8 Aprili 2017

MAFUNZO YA MAJAJI YAMALIZIKA NA KAMATI ZA USHAURI ZA JAJI MKUU ZAKUTANA

 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama  mara baada ya kumalizika kwa Mafunzo ya siku tano ya Majaji wa Tanzania yaliyohusu utendaji kazi hasa namna bora ya Kuimarisha Upatikanaji wa Haki kwa wakati pamoja na kuondosha Mashauri ya muda Mrefu Mahakamani

 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (katikati) akiwa kwenye Mafunzo ya Majaji yaliyomalizika jana jijini Arusha. Kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocakati na Kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Eva Nkya.
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma akifunga Mafunzo ya Siku tano ya Majaji wote wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Arusha.

 Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani na Mratibu wa Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Zahra Maruma akiwasilisha Mada kuhusu Maboresho ya Mahakama ya Tanzania wakati Kamati za Kumshauri Jaji Mkuu zilipokutana leo mjini Arusha.
 Majaji wa Mahakama ya Rufani na Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Ushauri za Jaji Mkuu Mhe. Shaaban Lila (kushoto) na Mhe. Kipenka Mussa (kulia) wakiwa kwenye Mkutano wa kamati za Ushauri leo jijini Arusha

 Jaji wa Mahakama ya Rufani Mheshimiwa Shaaban Lila akizungumza wakati wa Mkutano wa Kamati za Ushauri za Jaji Mkuu leo jijini Arusha
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati za ushauri za Jaji Mkuu leo wakati wa Mkutano wqa kamati hizo jijini Arusha.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Ushauri za Jaji Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Arusha,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni